Moja ya sababu ambazo watu wamekuwa wakizitumia kwamba
zinawazuia kufikia mafanikio ni kutokujua vitu fulani au kwa kuelewa zaidi
kutokuwa na uzoefu. Kwa kuwa mimi lengo langu ni kukuwezesha wewe kufikia
mafanikio makubwa, nahakikisha visababu hivi vinakosa nguvu na wewe unaanza
kufanyia kazi kile unachotaka kupata.
Sasa leo tuanze na vitu ambavyo huvijui. Kama kuna vitu hujui,
kama kuna vitu huna uzoefu navyo, kwanza hongera sana kwa sababu umedhibitisha
kwamba wewe ni binadamu. Kila mtu alizaliwa akiwa anajua kitu kimoja kikubwa,
jinsi ya ku “survive”, yaani jinsi ya kupona kwenye haya mazingira. Ndio maana
mtoto hata akizaliwa leo, anajua kunyonya na kulia pia ili kufikisha ujumbe
kwamba kuna kitu sio kizuri.
Lakini vitu vingine vyote kwenye maisha yako, ulizaliwa ukiwa
hujui na sasa unajua. Je kuna maajabu hapa, la hasha, ulijifunza. Ulizaliwa
hujui kusoma wala kuandika, ila sasa hivi upo hapa na unasoma makala hizi nzuri
zinazokupatia maarifa. Ulizaliwa ukiwa hujui lugha yoyote zaidi ya kulia, la kwa
sasa huenda unajua lugha sio chini ya tatu. Ulizaliwa ukiwa hujui kupika,
kuendesha chombo cha usafiri na vingine vingi ambavyo kwa sasa unafanya, lakini
uliweza kujifunza na sasa unavifanya.
Sasa kwa nini unatumia hicho unachoshindwa kufanya sasa kama
kigezo cha wewe kuacha kufanya au kama sababu ya kushindwa? Si unaweza kujifunza
kama ulivyojifunza hivyo vitu vingine?
SOMA; Umuhimu
Na Jinsi Ya Kujenga Uaminifu Kwa Wateja Wako.
Kama kuna kitu chochote ambacho unafikiri kwa kutokukijua
kinakuzuia kufikia mafanikio, jifunze kitu hicho. Tunaishi kwenye dunia ambayo
kujifunza kumerahisishwa sana. Kwa kutumia simu yao tu unaweza kujifunza
chochote unachotaka kujifunza. Tumia nafasi hii vizuri. Iwe unataka kujifunza
upishi, iwe kujifunza uandishi, iwe kujifunza lugha ya kigeni, iwe kujifunza
biashara na mengine mengi yanawezekana.
Wakati mwingine ukisema kwamba hujafikia mafanikio uliyotaka kwa
sababu hujui kitu fulani utakuwa unatudanganya, maana ukweli ni kwamba ulikuwa
na nafasi ya kujua ila hukuitumia vizuri. Anza sasa kuitumia nafasi hiyo.
TAMKO LA LEO;
Kitu chochote ambacho sikijui sio kikwazo kwangu kufikia
mafanikio, bali hiki ni kitu muhimu ninachotakiwa kujifunza ili niweze kufikia
mafanikio makubwa. Nitajifunza kila kitu muhimu ninachotakiwa kujua ili kufikia
mafanikio, kama ambavyo nimejifunza vitu vingine kwenye maisha.
Tukutane kwenye ukurasa wa 166 kesho, Like page yangu ya
Coach
Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha
kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365
bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo
maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya
facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya
email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na
KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata
utaratibu.
TUPO PAMOJA.