Lengo la kila makala ninayoandika, lengo la kila ujumbe
ninaoutoa wka njia mbali mbali iwe ni maongezi au hata video(angalia na jiunge na AMKA TV) ni kukupa wewe
maarifa na mbinu za kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi. Kwa kuwa hiki ndio
unachotaka kwenye maisha yako, au sio?

Leo nataka nikushirikishe baadhi ya vitu ambavyo usikubali
kabisa kujishikiza navyo kwenye maisha. Kwa kujishikiza na vitu hivi unajiandaa
kukatishwa tamaa na kuyafanya maisha yako kuwa magumu sana.

Tumewahi kujadili hapa kuhusiana na vitu tunavyokutana navyo
kwenye maisha. Na tukasema kila kitu ulichanacho au unachokutana nacho kwenye
maisha kinaingia katika moja ya makundi haya mawili. Kundi la kwanza ni vitu
unavyoweza kuviathiri au kuvidhibiti na kundi la pili ni vitu ambavyo huwezi
kuviathiri au kuvidhibiti.

Sasa leo nataka tujadili vitu ambavyo huwezi kuviathiri au
kuvithibiti. Vitu unavyoweza kuviathiri tulishavijadili kwenye makala hii; Kitu
Pekee Unachoweza Kukidhibiti Kwenye Maisha Yako.

Kwenye maisha yako usijishike na vitu ambavyo huwezi
kuvidhibiti, utajitengenezea nafasi kubwa ya kuumia moyo na kukatishwa tamaa.
Huwezi kudhibiti ni kwa muda gani familia yako na marafiki zako wataishi. Huwezi
kudhibiti ni kwamba utapandishwa cheo kazini au la. Huwezi kudhibiti kwamba kila
biashara utakayofanya lazima ufanikiwe. Huwezi kudhibiti kama mwenza au mchuma
uliyenaye mtakuwa pamoja mpaka kifo kiwatenganishe.

Hivi ni baadhi ya vitu vilivyopo nje ya uwezo wako wa udhibiti,
japo unaweza kutengeneza mazingira mazuri na kuwa na vitu hivyo. Lengo la
kujadili haya ni wewe kutouweka maisha yako yote katika vitu ambavyo huwezi
kuvidhibiti. Kujua kwamba lolote linaweza kutokea ambalo lipo nje ya uwezo wako
na likavuruga kila ambacho ulikuwa unaamini.

Hivyo furahia vitu kama vilivyo ila jua vinaweza kubadilika muda
wowote bila ya wewe kutaarifiwa.

TAMKO LA LEO;

Najua kuna vitu vingi kwenye maisha siwezi kuvidhibiti. Kuanzia
sasa sitoshikilia maisha yangu kwenye vitu hivi. Nitavifurahia wakati ninavyo na
nitafanya juhudi zilizopo ndani ya uwezo wangu kuvikuza viwepo, ila pale
vitakapoondoka kwa sababu ambazo siwezi kuzizuia nitajua ni sehemu ya maisha na
sitokata tamaa na maisha yangu.

Tukutane kwenye ukurasa wa 167 kesho, Like page yangu ya
Coach
Makirita Amani
uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha
kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365
bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo
maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya
facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya
email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na
KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata
utaratibu.

TUPO PAMOJA.