Kuna watu ambao wanakuwa wameanzia chini sana kwenye maisha.
Wanatokea kwenye familia masikini, wanaweka juhudi nyingi sana na hatimaye
wanafikia mafanikio waliyokuwa wanayatazamia. Ila baada ya kufikia mafanikio
haya wanashindwa kwenda tena mbele na wanabaki palepale. Kwa kubaki palepale kwa
muda mrefu wanajikuta wameachwa nyuma.

Kuwa wengine wanaingia kwenye kazi na wanaanzia ngazi ya chini
kabisa. Wanakuwa na hamasa kubwa ya kwenda ngazi za juu na hivyo kuweka juhudi
kubwa sana. Wanaweka juhudi hizi kweli na hatimaye wanafika ngazi za juu.
Wanapofika pale wanafikia kikomo na hawaendi tena mbele.

Tatizo kubwa linalokufanya unashindwa kwenda mbele zaidi ya hapo
ulipofika sasa ni kuendelea kufanya kile ambacho kimekufikisha hapo ulipo.
Sikiliza, kile kilichokufikisha hapo ulipo, ndio kitakufanya uendelee kuwa hapo
ulipo. Kama unataka kwenda mbali zaidi ya hapo ulipo sasa, unahitaji kufanya
kitu cha tofauti na unachofanya sasa.

SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutajirika Kwa Kuanza Na Shilingi Elfu
Moja.


Watu wengi wamekuwa wanafanya mambo kwa mazoea. Utawasikia, hivi
ndivyo nilivyofanya na nikafanikiwa, lakini ukweli ni kwamba mafanikio
wanayoongelea ni ya miaka mitano iliyopita. Kama mafanikio unayoongelea sio ya
wiki iliyopita au mwezi uliopita, tafadhali sana kaa kimya. Labda nirudie tena
kwa msisitizo, kama unajisifia kwa mafanikio uliyopata miaka miwili iliyopita
basi umeshapotea. Kama unajisifia kwa mafanikio haya ya mbali basi hakikisha una
mengine ya juzi juzi ya kusemea pia.

Adui wa wewe kwenda mbele zaidi ni hapo ulipo sasa, na anaanza
kwa kufanya vitu kwa mazoea kwa sababu ulishaozea kufanya hivyo. Mambo
yanabadilika kila mara, kilichokufikisha hapo hakitakupeleka mbele zaidi.
Unatakiwa kujua vipya na kuvifanyia kazi.

Kama bado hujasoma kitabu JINSI YA KUNUFAIKA NA MABADILIKO
YANAYOTOKEA, kisome sasa. Kukipata kitabu hiki tuma fedha tsh elfu 5 na email
yako kwenye namba 0717396253/0755953887 kisha utatumiwa kitabu hiki kizuri sana.
Usikose nafasi hii nzuri ya kunufaika na mabadiliko yanayoendelea kutokea kwenye
maisha yako ya kila siku na kuweza kufikia mafanikio makubwa.

TAMKO LA LEO;

Najua ya kwamba kilichonifikisha hapa nilipo, hakitaweza
kunifikisha mbali zaidi. Najua kutumia kile nilichozoea kufanya kufika mbele
zaidi ni kupoteza muda. Nahitaji kubadilika, nahitaji kuja na njia mpya kila
siku ili niweze kunufaika na mabadiliko yanayotokea kwenye
maisha.

Tukutane kwenye ukurasa wa 171 kesho, Like page yangu ya
Coach
Makirita Amani
uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha
kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365
bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya
facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na
KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata
utaratibu.

TUPO PAMOJA.