kuyafanya ili kuboresha maisha yako. Mambo haya yanahitaji wewe ubadilike, uanze
kufanya tofauti na ulivyozoea kufanya na sio kitu rahisi sana.
Kuacha kuangalia tv na kujisomea mambo yatakayokuweka mbele
zaidiinahitaji kujitoa kweli.
Kuacha kukaa na jamaa zako kila jioni mkipata moja moto na moja
baridi ili upate muda mwingi zaidi wa kuweka kwenye kazi au biashara yako sio
kitu rahisi.
Kuacha kulalamika pale unapoona kabisa kwamba umeonewa au
umeumizwa inahitaji nguvu ya ziada.
Kuacha usingizi na kuamka asubuhi na mapema sana ili uweze
kujifunza na kuipangilia siku yako sio kitu rahisi kama unavyoweza
kufikiria.
Tuseme labda wewe umeona kwamba mambo haya yote huwezi, kwa
sababu tu una uvivu uliopitiliza au kwa kifupi basi tu hutaki kujihangaisha. Leo
nataka nikuambie kitu kimoja muhimu sana cha kufanya.
SOMA; Kauli KUMI Za Marcus Aurelius Zitakazokufanya Uyaone Maisha Kwa
Utofauti.
Tafadhali sana hata kama una uvivu kiasi gani, jitahidi ufanye
kitu hiki kimoja na maisha yako yatagusa wengine kwa kiasi kikubwa sana.
Kitu chenyewe ni kuishi maisha mazuri kwako na kwa
wanaokuzunguka. Kuwa mtu mwema, usimwibie mtu, usisengenye mtu, usijihusishe na
majungu. Saidia wengine kadiri ya uwezo wako. Yaani kuwa tu mtu mwema na wengine
waone wewe ni mfano wa kuigwa. Na hata kama kuna mtu amekosa tumaini kwa kuyaona
maisha yako atapata tumaini kwamba dunia bado ina watu wema waliomo.
Hili ni jambo muhimu kwetu sote kufanya hata kama unafanya hayo
mengine yote unayojifunza kila siku.
TAMKO LA LEO;
Nitahakikisha naishi maisha ambayo yatakuwa mfano mzuri kwa watu
wengine. Nitajiepusha na mambo ambayo sio mazuri kwangu na kwa wale
wanaonizunguka. Sitoiba wala kumdhulumu mtu, sitosengenya wala kushiriki majungu
na nitasaidia wengine kadiri ya uwezo wangu.
Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita
Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi
yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365
bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo
maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya
facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya
email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na
KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata
utaratibu.
TUPO PAMOJA.