Tatizo la kushindana kwa bei kwenye biashara ni kwamba linawamaliza wote mnaoshindana.

Watu wengi huwa wanafikiri kwamba kwa kuweka bei ndogo basi ndio wanavutia wateja wengi. Hivyo wanaweka bei ndogo na mwanzoni wateja wanakuja kweli, baadae mshindani wako naye anashusha bei na wateja wanaenda kwake tena. Mnafanya mchezo huu kwa muda mpaka pale mnapojikuta wote mpo chini na hakuna anayetengeneza faida.

Hilo bado sio tatizo, kwani tatizo kubwa la kupunguza bei ni kwamba utashindwa kutoa huduma nzuri, utaajiri watu ambao unawalipa kidogo na hutakuwa na uwezo wa kuongeza chochote. Hivyo huduma zinakuwa mbovu na wateja wanaacha kujali.

Wateja wanapoacha kujali, biashara inashindwa kujiendesha na ndio inakuwa basi tena, unashindwa kuendelea na biashara.

Sasa ufanye nini kama ndio upo kwenye mashindano haya ya kuelekea kaburini? Au kama bado hujaingia ufanye nini?

Kwanza kabisa acha kushindana kwa bei na pia cha narudia tena kwa herufi kubwa ACHA KUFANYA KILE AMBACHO KILA MTU ANAFANYA. Kuwa tofauti, ongeza thamani na toa huduma bora sana kwa wateja wako. Kama unafikiri hili haliwezekani soma hapa na uone ni kweli huwezi au hutaki tu; Huwezi Au Hutaki? Kabla Hujaniambia Huwezi, Hakikisha Huponi.

Simama katika kundi la wafanyabiashara wengi ambao wanakimbizana mbio za kifo kwa kushusha bei, ongeza thamani zaidi kwenye biashara yako na hakikisha mteja anapata huduma ambayo hajawahi kuipata sehemu nyingine yoyote. Hii ndio silaha itakayokuwezesha kupambana na ushindani wa kwenye biashara.

Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.

Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.

Jiunge na COACHING/MENTORSHIP PROGRAM ambapo utapata muongozo wa hatua kwa hatua mpaka ufikie mafanikio kwenye kazi au biashara unayofanya. Bonyeza haya maandishi kupata maelekezo ya programu hii.