KITABU CHA JULY; THE SECRET CODE OF SUCCESS(Siri Ya Mbinu Ya Mafanikio)

Habari za leo mpenzi msomaji wa AMKA MTANZANIA, karibu tena kwenye utaratibu wetu wa kutumiwa vitabu vizuri vya kujisomea. Kila mwezi tumekuwa tunakutumia kitabu kimoja cha kujisomea ambacho kama utakisoma basi utajifunza mambo mazuri ambayo yataboresha maisha yako kama utafanyia kazi.
Kuna nini tena cha siri kwenye mafanikio pamoja na kusoma vitabu vingi? Huenda hili ni swali ambalo unajiuliza hasa kama umeshasoma vitabu vingi ambavyo nimekutumia. Ni muhimu sana pia kusoma kitabu hiki kwa sababu kuu moja.

Kitabu hiki cha THE SECRET CODE OF SUCCESS kimeandikwa tofauti kabisa na vitabu vingine vyote vinavyohusu mafanikio. Vitabu vingi vinakufundisha wewe ni JINSI GANI YA KUFANIKIWA(HOW TO) na watu wengi wamekuwa wanajifunza mbinu hizi na kuzifanyia kazi ila bado hawaoni majibu waliyotegemea kupata. Mwandishi wa kitabu hiki amekuja na njia ya tofauti na yeye anakuambia ni KWA NINI UFANIKIWE(WHY TO).
Mwandishi anatumia msingi wa akili yetu ambayo imegawanyika katika sehemu kuu mbili, sehemu ya kwanza ni akili inayofikiri kabla ya kufanya maamuzi(conscious mind) na sehemu ya pili ni akili isiyofikiri bali inahifadhi na kufanya kila kitu(subconscious mind). Mwandishi anasema conscious mind inamiliki asilimia 10 ya maamuzi yako yote na asilimia 90 inamilikiwa na subconscious mind.
Katika kila jambo unalotaka kufanya, akili yako huwa inapima kama lina faida au lina hasara. Hii haiishii hapo tu kwa sababu subconscious mind yako ina sababu nyingi sana za kwa nini huwezi na kwa nini utashindwa kuliko sababu za kwa nini unaweza.
Hapa ndipo mwandishi alipokuja na mbinu mpya ambayo itaweza kubadili zile sababu za kwa nini usifanikiwe na kuweka sababu nyingi za kufanikiwa. Mwandishi anasema hata watu waliofanikiwa, wengi wao hawajui kwamba kuna mambo wanayofanya kwa tofauti na wengine wanavyofanya na hii yote inatokana na jinsi ambavyo mawazo yao yako tofauti na watu wengine.
Mwandishi ametushirikisha mambo saba muhimu ya kufanya ili uweze kutoka hapo ulipo sasa na kwenda mbele zaidi kwenye mafanikio. Jifunze mambo haya saba na yafanyie kazi na hakika maisha yako yatabadilika. Sio mambo magumu, sio mambo mapya na wala huhitaji fedha za ziada ndio uweze kuyafanya. Ni wewe tu kuanza kubadili sehemu ndogo ndogo za maisha yako na kila kitu kinaanza kwenda vizuri.
Nisikumalizie uhondo wa kitabu hiki, tafadhali kipakue kwa kubonyeza maandishi haya ya kitabu THE SECRET CODE OF SUCCESS na uanze kusoma na kufanyia kazi yale ambayo umejifunza.
Tafadhali sana usiache kusoma kitabu hiki, ni muhimu sana sana kwako kukisoma. Najua nimekuwa nasema hivyo kwa kila kitabu lakini ni kwa sababu namaanisha kweli. Huwa sikupi kitabu kabla sijakisoma na unapoona nakupa kitabu kimoja jua nimesoma vitabu nane halafu kati ya hivyo nachagua kimoja ambacho kitakusaidia sana wewe msomaji wangu. Kila mwezi nasoma vitabu visivyopungua nane, angalau viwili kila wiki halafu nachukua kimoja ambacho na wewe unaweza kusoma na kunufaika.
Daudi Mwakalinga pia amefanya uchambuzi mzuri sana wa kitabu hiki, unaweza kuusoma na kujifunza mengi zaidi. Kusoma uchambuzi huo bonyeza maneno haya; Mambo 20 Niliyojifunza Kwenye Kitabu Kinachoitwa THE SECRET CODE OF SUCCESS.
Nakutakia kila la kheri kwenye usomaji wa kitabu hiki na jitahidi utoke na vitu angalau kumi ambavyo utavifanyia kazi. Karibu sana kama kuna chochote unachohitaji kuwasiliana nami, niandikie kwenye makirita@kisimachamaarifa.co.tz
TUPO PAMOJA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: