kipekee ila kila ulipopita mtaani ukaanza kuona karibu kila mtu anayo?
Au labda unafikiria kununua kitu fulani mfano gari au vifaa,
mara ghafla ukiwasha tv unaona kitu kile, ukipita mtaani unaona kitu
kile?
Au umewahi kufikiria kufanya biashara fulani mara ghafla ukaanza
kuona kila unapopita unaona watu wanafanya biashara ile?
Je unafikiri vitu hivyo nimeanza kutoke kwa sababu wewe
unafikiria kufanya? Jibu ni hapana, vitu hivyo vilikuwepo kila siku, ila kwa
sababu hujawahi kuvifikiria na kuvizingatia basi umekuwa huvioni. Ila unapoanza
kuvifikiria au kuvizingatia sana macho yako yanafunguka na unaanza kuona vizuri
zaidi.
SOMA; Huwezi Au Hutaki? Kabla Hujaniambia Huwezi, Hakikisha
Huponi.
Kuna fursa nyingi sana ambazo zinakuzunguka hapo ulipo. Ila kwa
sasa huzioni kwa sababu hujazingatia kuzifikiria. Anza kufikiria kitu fulani na
utaanza kuona kwamba kuna njia nyingi sana za kuweza kukipata au kukifanya kitu
hiko?
Unataka kuona fursa zaidi? Fungua akili yako, fungua mawazo yako
na macho yako yataanza kuona.
TAMKO LA LEO;
Najua nimekuwa sioni fursa nyingi kwa sababu macho yangu
hayajafunguliwa kuona. Nitayafungua sasa macho yangu kwa kuzingatia vitu
ninavyotaka, kuviweka kwenye akili yangu na macho yangu yatanionesha njia za
kufanya au kupata vitu hivyo.
Tukutane kwenye ukurasa wa 195 kesho, Like page yangu ya
Coach
Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha
kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365
bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo
maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya
facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya
email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na
KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata
utaratibu.
TUPO PAMOJA.