Katika shule moja kulikuwa na kundi la wanafunzi watukutu ambao
walikuwa wakionea wanafunzi wenzao. Wanafunzi hao walikuwa wakikuta mwanafunzi
mwingine wanamlazimisha achague wa kupigana naye na akikataa wanampiga
wote.

Siku moja kundi hili walikutana na mwanafunzi mmoja aliyeonekana
kuwa mnyonge sana. Wakamwambia achague wa kupigana naye. Yule mwanafunzi
akachora mstari na kusema yule ambaye anajiona ndio mbabe kuliko wote avuke huu
mstari. Yule ambaye ndio alikuwa mbabe alivuka mstari ule na alipofika upande wa
pili yule mwanafunzi mnyonge alimwambia sasa tupo upande mmoja, tuungane
kupambana na hao wengine.

Maisha ndivyo yalivyo, sisi wote tuko upande mmoja. Na watu wote
wanaokuzunguka mpo nao upande mmoja. Sema watu hatuelewi hili na ndio maana
tumekuwa tunashindana lakini hatufiki mbali.

Kama wanandoa wangejua kwamba wapo upande mmoja, wa kutaka
maisha yao wote kuwa bora basi matatizo mengi sana ya ndoa yasingekuwepo na ndoa
zingedumu.

Kama mwajiri na mwajiriwa wangejua wapo upande mmoja, kunufaisha
kazi yao na maisha yao kwa ujumla, basi kungekuwa na ufanisi mkubwa sana kwenye
eneo la kazi.

Kama mfanyabiashara na mteja wake wangejua kwamba wapo upande
mmoja basi biashara zingeendeshwa kwa mafanikio makubwa kwa wote wawili.

Lakini mara nyingi tunafikiri kwamba tuko pande tofauti na hivyo
kuishia kushindana, mashindano ambayo hayamfaidishi hata mmoja wetu.

TAMKO LA LEO;

Najua kwamba wale wote ambao wamenizunguka tupo upande mmoja.
Mwenza wangu, wateja wangu, mwajiri/mwajiriwa wangu wote tupo upande mmoja. Kila
mara nitajitahidi kuelewa upande tuliopo ili iweze kutusaidia kuboresha maisha
yetu sote.

Tukutane kwenye ukurasa wa 199 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita
Amani
uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi
yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365
bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo
maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya
facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya
email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na
KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata
utaratibu.

TUPO PAMOJA.