Umekuwa unatabiri mambo mengi sana kuhusu maisha yako, lakini je ni mambo mangapi uliyotabiri yametokea?

Ni mambo mangapi ambayo ulikuwa unayahofia, yanakunyima usingizi yametokea kweli? Nafikiri ni machache sana, kama hata yapo.

Kesho yako ni nzuri kama unavyoiona hapo kwenye picha.
Kesho yako ni nzuri kama unavyoiona hapo kwenye picha.

Ukweli ni kwamba wewe sio mtabiri mzuri, na wala hutakuwa mtabiri mzuri kadiri siku zinavyokwenda.

Umekuwa ukijitabiria kwamba maisha yatakuwa magumu zaidi, kwamba utapata hasara kwenye biashara, kwamba utafukuzwa kazi, kwamba mambo hayataenda vizuri!!

Lakini haya yote huwa yanatokea?

Hayatokei na hata kama yakitokea sio kwa sababu umetabiri ila kwa sababu umeamua kukubaliana na kile unachotabiri. Unatabiri kwamba utapata hasara kwenye biashara halafu unaendelea kuendesha biashara yako kwa mazoea, unaishia kupata kweli hasara.

Ninachotaka kukuambia leo ni kwamba chochote unachotabiri leo hakina maana, chochote unachohofia leo ni kupoteza muda wako. Hata ungetabiri kiasi gani na kujijaza hofu kiasi gani hakuna mmoja wetu anayejua nini kitatokea kesho.

Na hii ni vizuri sana kwa sababu lengo lako kubwa ni kuishi vizuri leo, kufanya kile ulichopanga kukifanya leo, kwa ubora wa hali ya juu sana kama vile ndio unakifanya kwa mara ya mwisho na hutakuwa na haja ya kuhofu kuhusu kesho tena.

Kwa sababu ukiishi vizuri leo, unaandaa mazingira mazuri ya kuishi vizuri kesho. Ukifanya kazi yako kwa ubora leo unaandaa mazingira mazuri ya kufanya kazi yako vizuri kesho. Ukimhudumia mteja wako vizuri leo, kwa huduma nzuri ambayo hajawahi kuipata sehemu nyingine yeyote, unafikiri kesho ataenda wapi?

Unaona mambo yalivyo mazuri sasa? Huna haja ya kutabiri, huna haja ya kuhofia, weka nguvu zako kwenye kufanya kilicho bora leo, sasa hivi wakati bado una nafasi hiyo ya kufanya hivyo.

TAMKO LA LEO;

Nimekuwa mtabiri kwa kipindi kirefu sana kwenye maisha yangu. Nimekuwa natabiri vitu vingi ambavyo havijawahi kutokea. Nimegundua sasa ya kwamba nilikuwa napoteza muda wangu mzuri kwenye utabiri huu na kujijaza hofu. Sasa nimeamua kuachana na utabiri huu usio na maana kwangu na nitaishi vizuri leo, sasa hivi wakati bado nina nafasi hii. Vile nitakavyoishi leo ndio utabiri wa kesho.

Tukutane kwenye ukurasa wa 201 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Pia usiache kutembelea mtandao huu kila siku kujifunza mambo mapya na mazuri. Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.