Biashara unayofanya sasa, haitakuwa hivyo ilivyo kwa miaka kumi ijayo. Japo kipindi hiko kuna watu ambao bado watakuwa wanaifanya kama inavyofanywa sasa. Ila hawa ni wale ambao wanaendesha biashara za kawaida, zinazowaumiza vichwa na zisizo na faida kubwa.

UMESHAJUA PA KUTOROKEA?
UMESHAJUA PA KUTOROKEA?

Wajanja wote kwenye biashara wajua mlango wa kutorokea na wakati wakutoroka.

Bado hujanielewa vizuri namaanisha nini ninaposema utoroke?

Namaanisha kwamba kuna wakati utahitaji kubadili biashara yako au hata kuondoka kabisa kwenye biashara hiyo. Ngoja twende kwa mifano utanielewa vizuri zaidi.

Wakati hizi biashara za kutuma na kuweka fedha kwa njia ya simu, zilikuwa na faida kubwa sana, zilifanywa na wachache na waliweza kuendesha biashara zinazojitegemea. Ila kadiri siku zinavyokwenda biashara hizi zinakutana na changamoto nyingi sana. Na watu wote wanaojua biashara wanazikimbia biashara hizi au kuzifanya kutokuwa biashara kuu.

Wakati boda boda zinaingia ilikuwa ndio habari ya mjini. Kuna watu waliuza mashamba na kwenda kununua boda boda. Kuna watu walichukua mafao yao na kwenda kununua boda boda. Mtu aliweza kuwa na boda boda mpaka 50 na kwa wiki anapata mahesabu yake mazuri na maisha yanaenda vizuri. Ila kwa kipindi hiki, kuwa na boda boda 50 unaweza ukalazwa hospitali kwa presha. Biashara hii imekuwa na changamoto nyingi sana, na waliozioana mapema waliondoka a kuingia kwenye biashara nyingine.

Na wewe ndivyo ilivyo kwenye biashara yako, usifikiri utaendelea kufanya biashara yako kwa mtindo huo huo kwa miaka kumi ijayo, hakuna kitu kama hiko. Labda kama unajiandaa kushindwa.

Unachotakiwa kufanya ni wakati upo kwenye biashara uliyopo sasa, angalia ni jinsi gani unaweza kuibadili na au kuijumuisha na biashara nyingine(mlango wa kutoroka). Na pia jua wakati ambapo ni sahihi kufanya hivyo(wakati wa kutoroka). Naita kutoroka kwa sababu ni wachache sana wanaoelewa mbinu hii, na wewe umeshaielewa sasa. Ifanyie kazi.

MUHIMU SANA; Soma kitabu jinsi ya kunufaika na mabadiliko yanayotokea, kitakuandaa vizuri sana na mabadiliko yanayoendelea kwenye biashara yako. Kukipata bonyeza maandishi haya.

Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.

Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa.

Kama una swali au changamoto yoyote ya kibiashara au kijasiriamali basi iweke kwenye FORUM YETU YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI. Bonyeza hayo maandishi kuuliza swali lako na utapata michango kutoka kwa wengine. Karibu sana.

Jiunge na COACHING/MENTORSHIP PROGRAM ambapo utapata muongozo wa hatua kwa hatua mpaka ufikie mafanikio kwenye kazi au biashara unayofanya. Bonyeza haya maandishi kupata maelekezo ya programu hii.