Kwenye uchumi kuna nadharia moja inaitwa ZERO-SUM-GAME. Kwa nadharia hii ni kwamba mmoja akipata, mwingine anakosa.
Kuna kipindi nadharia hii ilikuwa inaaminika na wengi na hivyo watu kuchukiana na hata kuingia kwenye matatizo makubwa.


Kwa mfano watu walikuwa wanaamini kwamba ili uwe tajiri lazima wengine wawe masikini. Au kama wewe ni masikini basi umasikini wako umesababishwa na matajiri wanaokuzunguka. (bado unaamini hivi?)
Ukweli ni kwamba nadharia hii sio sahihi hasa kwenye maisha ya kawaida, kazi, biashara na mafanikio. Sio kweli kwamba ili wewe upate lazima mwingine akose. Sio kweli kwamba waliopata ndio wamefanya wewe ukose.
Sio kweli kwamba ili wewe uwe na furaha ni lazima mwingine apate maumivu.
Sio kweli kwamba ili wewe ufanikiwe ni lazima mwingine ashindwe.
Sio kweli kwamba ili wewe ufaulu ni lazima mwingine afeli.
Kuna fursa nyingi sana hapa duniani zinazotuwezesha wote kupata, na sio kugombania vichache ambavyo vinaonekana.
Kwa mfano mtu mmoja anafikiria biashara, inakuwa na faida na wengine wanamwiga yeye, baada ya hapo wanaanza kugombania wateja wachache wanaokuja. Badala ya wewe kuingia kwenye mchezo huu fikiri njia ya tofauti ambayo haipo ambayo itakupatia kile unachotaka, na wakiiga tena badilika hivyo hivyo.
Kuna fursa nyingi sana ambazo zinakuzunguka sasa. Huna haja ya kuingia kwenye ushindani ambao hautakuwa na faida kwako.
Mimi ni mmoja wa watu ambao wanapinga sana ushindani wa kugombania kitu kimoja kama vile ndio kitu pekee kilichopo. Fikiria zaidi, fursa zipo nyingi sana.
TAMKO LA LEO;
Najua kwamba kuna fursa nyingi sana kuliko ambazo watu wanazitolea macho sasa. Najua watu wengi wana mtizamo kwamba fursa zilizopo ndio pekee za kugombania. Mimi najua fursa zipo nyingi sana. Nitaendelea kuibua fursa zitakazonifanya niwe tofauti na zitakazoniletea mafanikio makubwa.
Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Pia usiache kutembelea mtandao huu kila siku kujifunza mambo mapya na mazuri. Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.