Unajua ni kitu gani kinachokufanya unaendelea kufanya kile ambacho umepanga kuacha kufanya? Moja tu, sio mbaya.

Umeamua kwamba hutaki tena kunywa pombe, lakini unapita karibu na baa au unakutana na marafiki zako wanakunywa, na wanakuambia kunywa moja tu, sio mbaya, hutakufa na wala hutaharibu chochote. Lakini moja tu inapelekea nini???

Unapanga kwamba utakuwa unafanya mazoezi kila siku, unaanza kwa hamasa kubwa lakini baada ya muda unaanza kupata uvivu, unajiambia nikiacha siku moja tu sio mbaya. Lakini ni nini kinatokea baada ya hapo?

Unapanga kuamka asubuhi na mapema ili uweze kupangilia siku yako na hata kujisomea. Unaweka simu yako au saa ikuamshe asubuhi hiyo. Inakupigia kelele uamke, lakini wewe unasema wacha niongeze dakika kumi tu sio mbaya. Ni nini kinatokea baada ya kuongeza dakika hizo kumi?

UNAISIMAMISHA KWA DAKIKA TANO TU, UNAKUJA KUSTUKA NUSU SAA BAADAE, UMEPOTEZA.
UNAISIMAMISHA KWA DAKIKA TANO TU, UNAKUJA KUSTUKA NUSU SAA BAADAE, UMEPOTEZA.

Unaposema na kukubaliana kwamba moja tu sio mbaya jua ya kwamba umekubali kuvuruga kila ulichopanga kufanya. Unapoanza hata kwa kiwango kidogo sana tayari itavuruga kila kitu na hutaweza kwenda tena na mipango yako kama ilivyokuwa.

Unahitaji nidhamu kubwa ili uweze kufanikisha jambo lolote kwenye maisha yako. Kama utakosa nidhamu utakubaliana na haya mawazo ya moja tu sio mbaya na mawazo haya hayatakufikisha popote.

TAMKO LA LEO;

Najua kusema kwamba kuharibu mara moja tu sio vibaya, ni kuamua kuharibu mipango yangu yote kwenye maisha. Kuanzia sasa nitakataa kufanya hata kitu kidogo kinachoniondoa kwenye malengo yangu kwa kisingizio kwamba mara moja sio mbaya. Najua nidhamu ni moja ya misingi muhimu sana ya mafanikio. Na sehemu muhimu ya kutumia nidhamu ni kuepuka hivi vishawishi vidogo vidogo.

Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Pia usiache kutembelea mtandao huu kila siku kujifunza mambo mapya na mazuri. Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.