Habari za leo msomaji na rafiki yangu wa karibu.

Nina furaha kubwa sana kwa sababu tatizo lililokuwa linaendelea kwenye blog hii KISIMA CHA MAARIFA limetatulika.

MFANO WA FURAHA NILIYONAYO, HA HA HAA
MFANO WA FURAHA NILIYONAYO, HA HA HAA

Tangu tumebadili baadhi ya mifumo kwenye blog hizi kumekuwa na tatizo kubwa sana kwa watu kuweza kuingia na kusoma. Kila siku nilikuwa napokea malalamiko kutoka kwa wasomaji ambao wanafika kwenye blog wakitaka kusoma makala wanaambiwa NOT FOUND.

Tatizo hili liliniumiza kichwa sana, tuliweza kutatua nusu na bado wasomaji wanaotumia opera mini wakawa hawawezi kusoma. Tuliendekea kufanyia kazi changamoto zote hizi na hatimaye sasa nafurahi kwamba tumeweza kutatua tatizo.

Sasa hivi kila msomaji anaweza kusoma makala kwenye blog bila ya kupata changamoto yoyote ile.

Naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa wasomaji wote kwa kuendelea kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki ambapo kulikuwa na changamoto ya usomaji. Hakumkata tamaa, mliendelea kutembelea tena na tena. Hii ni imani kubwa sana mmeonesha kwetu na tunalazimika kuendelea kuwahudumia vyema kw akuwapatia maarifa bora yatakayoweza kuyafanya maisha yetu sote kuwa bora zaidi.

Katika kipindi chote hiki cha changamoto sikuweza kuandika makala nyingi ambazo nilitarajia uzisome. Na pia baadhi ya mipango tuliyokuwa nayo ya mabadiliko haikuweza kutekelezeka. Ilibidi kutatua tatizo kwanza na sasa limekwisha.

ZAWADI KUBWA KWAKO MSOMAJI.

Kuna zawadi kubwa sana kwako kutoka kwenye mtandao huu. Kwa sasa utakuwa unaianza siku yako kwa makala nzuri za kurasa. Makala za kurasa zitakuwa zinakwenda hewani asubuhi sana na mapema sana ili wewe ukiamka tu kitu cha kwanza kufanya ni kuingia kwenye KISIMA CHA MAARIFA na kupata kitu bora cha kuanza nacho siku yako.

Kitu cha kwanza kabisa nitakachokuwa nafanya nikiamka ni kuandika makala ya UKURASA na kwenda hewani muda huo huo, natarajia kama mambo yatakuwa yanakwenda vizuri(hasa kwa upande wa mtandao) makala itakuwa hewani kila siku kabla ya saa kumi na nusu asubuhi. Kwa sababu naamka saa kumi kamili asubuhi na moja kwa moja naandika, kama mtandao unakuwa sawa, kutegemea na eneo nilipo kwa siku hiyo, makala itakwenda hewani mapema sana. HII NI KILA SIKU, HAIJALISHI MWISHO WA WIKI AU SIKUKUU.

NINACHOKUOMBA UFANYE.

Kikubwa ninachokuomba ufanye ni kila siku asubuhi, unapoamka kitu cha kwanza kabisa ingia kwenye KISIMA CHA MAARIFA, na upate mtazamo na wazo jipya la kuianza siku yako. Na kabla hujalala pia pitia KISIMA CHA MAARIFA upate makala nyingine nzuri zitakazowekwa kila siku. Pia usisahau kupitia AMKA MTANZANIA, kila siku ili kujifunza zaidi.

Pia nakuomba uwashirikishe watu wengine makala nzuri unazozisoma hapa. Na kama bado hujajiunga, lipia ada ya uanachama(elfu 30 au elfu 50 kwa mwaka) ili upate makala nzuri zilizopo na zitakazoendelea kuwekwa kwenye mtandao huu.

Makala za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 zitaendelea kupatikana bure kwa wote. Makala nyingine ikiwepo za UJUMBE LEO, na BIASHARA LEO zitapatikana kwa wanachama waliojiunga na kulipia ada.

Nategemea kuwa natoa maarifa mazuri sana kwenye makala hizo za UJUMBE LEO na BIASHARA LEO, usikubali kupitwa na vitu hivyo vizuri. Jiunge mapema na lipia ada yako ya uanachama.

Nashukuru tena sana kwa kuendelea kuwa pamoja nasi, tunaahidi kuendelea kuwa pamoja nawe siku zote, kwani safari hii haina kikomo, utaendele akujifunza kila siku katika maisha yako yote yaliyobakia.

Like page yangu facebook ili tuwe karibu zaidi, BONYEZA HAPA KULIKE PAGE.

Pia karibu kwenye kundi hili la facebook ambapo utajifunza mengi zaidi, BONYEZA HAPA KUINGIA KWENYE KUNDI.

Rafiki na KOCHA wako.

Makirita Amani.