Sababu ni moja, wivu.
Watu wanasema kuna wivu wa maendeleo na wivu usio wa maendeleo. Sijui tofauti zake sana, ila ninachojua wivu ni wivu.
Wivu ni nini basi? Kwa ninavyoelewa mimi mwenyewe wivu ni ile hali ambapo unamwona mtu mwingine ana kitu ambacho huna, halafu ukajisikia vibaya kwa nini na wewe huna kitu kile. Na mara nyingi mtu utajikuta unamchukia mtu yule ambaye ana kitu ambacho wewe huna.
Mwingine atasema wivu ni kuona mtu ana kitu fulani na wewe kutaka kitu kama kile. Labda, sijui.
Tukirudi kwenye uhalisia, na hapa tunaweka unafiki pembeni, ni kwamba kuna wakati unajisikia vibaya kuona mtu ana kitu fulani ambacho wewe huna. Wakati mwingine unaona mtu huyo hakufikii hata wewe kwa uwezo na juhudi, lakini kwa nini yeye ndio anakubalika zaidi?

Labda wewe ni msanii, unafikiria mbona huyu mwanamuziki anayeonekana maarufu nyimbo zake sio nzuri kama za kwangu?
Au wewe ni mfanyabiashara na unashangaa kuna mfanyabiashara mwingine, hana uwezo kama wako lakini ndio ana wateja wengi kila siku.
Au upo kazini nakuna mfanyakazi unajua kabisa uwezo wake ni mdogo lakini kila zikitokea nafasi nzuri anazipata yeye.
Unafikiri ni haki yako kuwa na wivu huu?
Ukweli ni kwamba kwa kuwa na wivu kunakuzuia wewe kupata kile ambacho wale unaowaonea wivi wanacho.
Yaani ni hivi kama unamwonea mtu wivu kwa sababu ana kitu fulani, unajizuia wewe kupata kitu hiko.
Kwa sababu gani? Kwa sababu kwa wivu yako unaiambia akili yako kwamba kile kitu ambacho mwenzako anacho ni kibaya na hivyo utafanya kila jitihada kukiepuka. Hutajua kama unafanya hivyo lakini itatokea yenyewe, akili yako itakuepusha na fursa zote zinazoweza kukuletea kitu kile.
Kadiri unavyozidi kuwa na wivu ndivyo unavyozidi kuwa na maisha magumu.
Ufanye nini basi?
Umeona mtu ana kitu ambacho na wewe ungependa kuwa nacho? Mbariki, furahia uwepo wake, mwombee azidi kufanikiwa zaidi. Kwa kufanya hivi unaifungua akili yako ili ikutengenezee fursa kama zile alizonazo mtu yule.
Mbariki aliyefanikiwa, na wewe utafanikiwa.
TAMKO LA LEO;
Nimejua kwamba kwa kumuonea mtu wivu najizuia mwenyewe kufanikiwa. Kila ninapoona wivu kwa mtu naondoa fursa zangu za kupata kitu kile. Kuanzia sasa nitawafurahia, kuwabarini na kuwaombea wale wote wenye mafanikio kuliko mimi ili na mimi niweze kufikia mafanikio makubwa.
Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Pia usiache kutembelea mtandao huu kila siku kujifunza mambo mapya na mazuri. Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.