image

Dunia imeshakupa kila kitu ambacho wewe unataka.
Kama unabisha angalia ni watu wangapi ambao wameanzia pabaya kuliko wewe lakini wameweza kufika mbali.
Sasa na wewe unawezaje kufika mbali zaidi ya ulipo sasa?
Acha kulalamika kwamba dunia haina usawa,
Acha kulalamika kwamba kuna wengine wanapendelewa,
Amua ni kitu gani unachotaka kwenye maisha yako,
Kifanyie kazi kwa juhudi na maarifa,
Kuwa mwaminifu,
Kuwa mwadilifu,
Kuwa na nidhamu.
Hakuna kitakachokushinda.
Rafiki na Kocha wako
Makirita Amani