Unaweza kutoa majibu au unaweza kutoa sababu, lakini sio vyote kwa pamoja, na pia havina uzito sawa.

Watu wengi tunapenda kutoa sababu, kwa sababu tunajua tukiwa na sababu tutasamehewa kwa kile ambacho tumeshindwa kufanya.

UNAWEZA KUTOA MAJIBU AU UNAWEZA KUTOA SABABU, SIO VYOTE KWA PAMOJA.
UNAWEZA KUTOA MAJIBU AU UNAWEZA KUTOA SABABU, SIO VYOTE KWA PAMOJA.

Hivyo wakati unafanya kitu, tayari unatengeneza na sababu, kama itatokea ukashindwa. Tayari unakuwa na sababu ya kutueleza. Hata hivyo nimeshindwa kwa sababu…. na hapo unatujazia sababu bora kabisa kuwahi kutokea duniani. Na huenda tukakusikiliza.

Japokuwa watu watasikiliza sababu zako, japokuwa watu wataonekana kukuonea huruma kwa sababu ulizotoa, lakini hili halitakufanya wewe kuwa shujaa. Watu wanapenda majibu na sio sababu. Dunia inatukuza majibu.

Majibu ni adimu, sababu zipo na kila mtu anaweza kuzitoa. Siku zote vitu adimu ndio vinakuwa na thamani kubwa. Na ndio maana majibu yanathaminiwa sana.

Kuliko kutoa sababu ni afadhali kukaa kimya na kuendelea kufanyia kazi kile unachofanya mpaka utakapokuja na majibu. Na uzuri wa majibu ni kwamba yanaonekana, huna haja ya kutumia nguvu nyingi kuyaeleza. Wewe fanya na sisi tutaona majibu. Au tafuta sababu nzuri za kutuambia kwa nini umeshindwa kuja na majibu, na tutakuona wewe ni mmoja ya kundi kubwa la watu ambao hawawezi kuja na majibu.

TAMKO LA LEO;

Najua ya kwamba naweza kutoa majibu au kutoa sababu, lakini siwezi kutoa vyote kwa pamoja. Na pia nimejua ya kwamba majibu yana thamani kubwa kuliko sababu. Hakuna mtu atakayekumbuka sababu zangu baadae, ila kila mtu atakumbuka na kufurahia majibu niliyoleta. Kuanzia sasa nitaacha kutafuta sababu na badala yake kuweka juhudi ili kutoa majibu mazuri na yatakayowasaidia wengi zaidi.

Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Pia usiache kutembelea mtandao huu kila siku kujifunza mambo mapya na mazuri. Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.