Kama unafanya kazi yoyote kubwa inayochochea mabadiliko kwa wengine, hongera sana.

Ni kazi nzuri lakini ni ngumu na hivyo inahitaji moyo sana, vinginevyo ni rahisi sana kukata tamaa.

MABADILIKO NI MAGUMU, LAKINI LAZIMA YAFANYIKE. HAKUNA KINACHOWEZA KUDUMU MILELE.
MABADILIKO NI MAGUMU, LAKINI LAZIMA YAFANYIKE. HAKUNA KINACHOWEZA KUDUMU MILELE.

Kama tunavyokubaliana, kwanza huwezi kumbadili mtu yeyote, watu hawapendi kubadilishwa, bali wanabadilika wenyewe. Hivyo lengo lako wewe sio kuwalazimisha watu wabadilike, ila kuwaonesha kwamba wanaweza na wanahitaji kubadilika. Halafu wanabadilika na maisha yao yanakuwa bora.

Sasa kuna changamoto mbili kubwa utakazokutana nazo wakati unakazana kuleta mabadiliko.

Changamoto ya kwanza ni watu ambao wanabadilika haraka/upesi. Unaweza kuona hawa ni rahisi na kazi sio kubwa, ila wanavyobadilika haraka/upesi jua pia ni vigumu kudumu na mabadiliko hayo. Ni rahisi watu hawa kubadilika tena na kuacha kile kizuri ambacho uliwafanya wabadilike.

Changamoto ya pili ni watu ambao kwamwe hawatabadilika. Hawa ni watu ambao hata kama ungefanya nini, hawawezi kubadilika. Yaani watu hawa wameshaamua maisha yao yawe vile yalivyo na hawawezi kukusikiliza hata kama ungewaambia nini.

Jua makundi haya mawili na unapokutana nayo, fanya maamuzi ya kusonga mbele haraka ili usipoteze muda wako.

Changamoto hizi zipo kwenye mabadiliko yoyote utakayotaka kuleta, iwe ni kushawishi wateja, kutoa elimu, kuhamasisha upigaji kura, kuhubiri dini na kingine chochote ambacho kinahitaji watu wabadilike.

Kwa mwanzo achana na makundi haya mawili na tafuta wale ambao kweli wataiona thamani ya mabadiliko, na huenda hawa wakibadilika, wengine wataona inawezekana kubadilika. Ila sio jukumu lako kuhangaika na makundi haya mawili.

N;B Kama bado hujasoma kitabu jinsi ya kunufaika na mabadiliko mpaka sasa unaweza kuwa kati ya makundi hayo mawili na ujumbe huu ukawa umepotea kwako. Kwa nini usikisome leo? tuma tsh elfu tano kwenye namba 0717396253/0755953887 na utume email yako kisha utatumiwa kitabu hiki. Kiko kwa pdf na unaweza kusomea kwenye simu au kompyuta.

TAMKO LA LEO;

Najua ya kwamba mabadiliko sio kitu rahisi kutokea. Japokuwa nataka kuleta mabadiliko kwenye biashara yangu, kazi yangu na hata kwa wale wanaonizunguka kwenye maisha, najua kuna watu ambao wanabadilika haraka sana na hawa hawawezi kudumu na mabadiliko. Na pia kuna wengine ambao hawawezi kubadilika kabisa. Nitatunza nguvu zangu kwa kuepuka watu wa aina hizi mbili ili niweze kuwafikia vizuri wale ambao wanaijua thamani ya mabadiliko na wako tayari kuyaishi mabadiliko hayo.

Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Pia usiache kutembelea mtandao huu kila siku kujifunza mambo mapya na mazuri. Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.