Siku sio nyingi wanaokuambia kwamba huwezi wataachana na wewe na kuendelea na maisha yao, au kutafuta mtu mwingine wa kumwambia hivyo.

Siku sio nyingi wanaokunyooshea kidole watachoka na kuendelea na mambo yao mengine.

USIPOKATA TAMAA WANAOKUKATISHA TAMAA WATAKATA TAMAA WENYEWE.
USIPOKATA TAMAA WANAOKUKATISHA TAMAA WATAKATA TAMAA WENYEWE.

Siku sio nyingi wanaokuambia utajuta kwa maamuzi uliyofanya watachoka kuendelea kukuambia hivyo na watatafuta mambo mengine ya kufanya.

Siku sio nyingi kazi yako itajisemea yenyewe hata kama wewe hutasema chochote.

Siku sio nyingi yale mabadiliko makubwa unayotaka yatokee kwenye maisha yako yatajidhihirisha.

SOMA; Unapokata Tamaa Maana Yake Umekubali Hivi.

Haya yote yatatokea siku sio nyingi kuanzia leo, lakini inahitaji uvumilivu wako ili uweze kufikia siku hizo.

Wanaokupinga wanaweza kuonekana wamepania kweli, ila wewe umepania zaidi yao na ndio maana watakimbia wakuache wewe ukifanyia kazi ndoto zako.

Usikate tamaa mapema, siku sio nyingi mambo yatakuwa mazuri na maisha yako yatakuwa bora sana. Haya yote ni kama utaendelea kufanya kile ambacho umechagua kufanya.

TAMKO LA LEO;

Najua ya kwamba hakuna anayejali maisha yangu kuliko ninavyoyajali mimi mwenyewe. Kuna watu wanaweza kuonekana wananikatisha tamaa ila najua hawawezi kudumu kwa hilo. Mimi pekee ndio ninayeweza kudumu kwenye mabadiliko haya makubwa niliyochagua kwenye maisha yangu. Najua siku sio nyingi vikwazo vyote vitadondoka na mambo yangu yatakwenda vizuri sana. Nitaendelea kuweka juhudi kila siku kwa sababu najua siku sio nyingi mambo yatakuwa mazuri.

Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Pia usiache kutembelea mtandao huu kila siku kujifunza mambo mapya na mazuri. Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.