Ni kiasi gani una uhuru?
Kama ulikuwa hujajua basi uhuru wako unaweza kupimika.
Unaweza kuupima uhuru wako kwa idadi ya siri ulizonazo, kwa vitu ambavyo unajaribu kuficha.

Kadiri una siri nyingi ambazo hutaki watu wajue, ndivyo uhuru wako unavyozidi kuwa mdogo.
Kadiri ambavyo unajaribu kuficha vitu vingi, ndivyo ambavyo unakosa uhuru wa kuishi na kufurahia maisha.
Na siri unayoficha inapokuwa inajulikana na baadhi ya watu, basi nao wanakuwa wameshikilia uhuru wako na watakunyanyasa pia.
Kuongeza uhuru wako, punguza siri ambazo unashikilia, punguza mambo ambayo unaficha.
Watu wanapokosa siri ya kukunyanyasa nayo, unakuwa na uhuru mkubwa sana kwenye maisha yako. Ila wanapokuwa na kitu kikubwa ambacho unajaribu kuficha, mara kwa mara watakitumia kukutishia ili uwape chochote wanachotaka.
Kama utafanya mambo yako kwa uaminifu na uadilifu. Kama utakuwa na misingi yako kwenye maisha na ukaisimamia, basi hakuna siri zozote utakazokuwa unajaribu kuficha, na hii itakuletea uhuru mkubwa sana, na utayafurahia maisha yako, na utafikia mafanikio makubwa.
TAMKO LA LEO;
Najua ya kwamba uhuru wangu utakuwa mkubwa kama sitakuwa na siri au vitu ambavyo najaribu kuvificha. Kuanzia sasa nitafanya mambo yangu kwa uwazi na kama jambo litahitaji kuwa la siri au kificho nitaachana nalo. Kwa sababu haijalishi ni zuri kiasi gani, baadae litatumika kuninyanyasa. Nitafanya mambo yangu yote kwa uaminifu na uadilifu.
Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Pia usiache kutembelea mtandao huu kila siku kujifunza mambo mapya na mazuri. Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.