Moja ya vitu vinavyowarudisha watu wengi nyuma ni kauli za watu ambao wanasemana kujidai wanajua sana.
Umeamua kufanya kitu cha tofauti na wao wanakuambia tunajua huwezi kufikia kitu hiko, tumeshaona wenzako kama wewe wakijaribu na kushindwa vibaya.
Kwa kukosa uzoefu na kujiamini watu wengi wamekuwa wanachukua kauli hizi kama sheria na hivyo kufukia kabisa ndoto zao.

Lakini ukweli ni kwamba hakuna anayejua kwa hakika ni nini kitakachotokea saa moja ijayo, kesho, wiki ijayo, mwezi ujao au hata mwaka ujao. Hakuna mtu wa aina hiyo, mwenye kueleza kwa uhakika kwamba kitatokea hivi na hivi na hivi na vyote vitokee.
SOMA; UKURASA WA 84; Pata Muda Wa Kuishi.
Wengi wa wanaoonekana wanajua wamekuwa wakibahatisha tu hapa na pale lakini hawawezi kurudia tena na kupata majibu yale yale. Kwenye sayansi tunasema kama umefanya kitu na kufanikiwa, lakini kitu hiko hakiwezi kurudiwa na wewe mwenyewe au mtu mwingine na akapata majibu kama uliyopata wewe basi kitu hiko sio cha uhakika.
Hakuna hata mmoja wetu anayejua ni nini hasa kitakachotokea kwa wakati ujao. Lakini unapoweka juhudi zako na kufanya kilicho bora, una nafasi kubwa zaidi ya kupata mafanikio makubwa kuliko ambaye hafanyi hivyo. Na hii ni furaha kubwa sana kwetu kwa sababu yote ambayo tunapigiwa kelele na watu kumbe hayana uhakika na sisi wenyewe tukiweka juhudi tuna nafasi ya kufanya vizuri sana.
TAMKO LA LEO;
Nimejua ya kwamba hakuna mwenye kujua kwa hakika ni nini kitakachotokea muda unaokuja. Wengi wa wanaonikatisha tamaa na kuniambia siwezi kumbe hata wao wenyewe hawana uhakika na kile wanachosema. Kuanzia sasa nitajipanga vizuri na kuweka juhudi kubwa bila ya kujali watu wanasema nini kuhusiana na siku zijazo. Najua kwa mipango yangu mizuri na juhudi zangu kubwa, najiweka kwenye nafasi nzuri ya kufikia mafanikio makubwa.
Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Pia usiache kutembelea mtandao huu kila siku kujifunza mambo mapya na mazuri. Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.