Jinsi Ulivyo Unajikubali Katika Kujiletea Mafanikio Makubwa?

Habari za leo rafiki yangu na mpenzi msomaji wa AMKA MTANZANIA, naamini umeuanza mwezi vizuri ukiendelea kujiimarisha kwa bidii eneo ulipo, iwe kwenye biashara yako ama kazini kwako ulipoajiriwa ama kwenye masomo yako. Hayo yote ni mazuri na unahitaji kuwa mwangalifu sana maana pale utakapoanza kujilinganisha na wengine na wewe ikatokea bahati mbaya ukaanguka utajiona hufai. Hebu tuangalie hii mada kuhusu uumbaji wako ulivyo na unatakiwa ujikubalije pale unapojikuta una tofauti na wenzako katika maumbile ya kimwili yaani viungo vya mwili na uwezo wako wa akili yaani kufikiri na kuchambua mambo unakuwa tofauti.

NICK VUIJICIC MTU ALIYEZALIWA BILA MIKONO WALA MIGUU LAKINI NI MHAMASISHAJI MKUBWA WA WATU KUFURAHIA MAISHA.

 
Kabla sijafika mbali katika kujadili hili naomba nikupe kwanza angalizo, ninachokijadili hapa kuhusu kujikubali ulivyo siyo ile hali ya kujikubali jinsi ulivyo mvivu, mwongo, mwizi na mengine mengi yanayofanana na hayo. Mimi ninachokizungumzia hapa ni vile ulivyozaliwa ukajikuta una ulemavu kwenye mwili wako, ukajikuta huna baadhi ya viungo vya mwili, unajikuta wewe ni mwanaume lakini una sauti ya kike tofauti na jamii zetu tulivyozoea, wewe ni mwanamke lakini una sauti ya nne na ndevu juu tofauti na jamii ilivyozoea kuwa mwanamke ni mtu laini asiye na makorombwezo mengi kwenye mwili wake, ama katika mizunguko yako ya maisha ukapata ajali mwili wako ukaharibika vibaya, ukapoteza baadhi vya viungo, ngozi yako ikaharibika vibaya wakati wewe hujazoea hiyo hali maana umezaliwa ukiwa mzima wa afya kabisa, ikatokea pia ukapata ugonjwa ambao unakuwa kama ndio sehemu yako ya maisha, unakuwa unaishi kwa kumeza dawa ama kuchomwa sindano za kukupa nguvu ili uendelee kuishi.
SOMA; Kama Unajibebesha Mizigo Hii Katika Maisha Yako, Sahau Kuhusu Mafanikio.
Hizi hali nilizozifafanua kwa kifupi hapo juu unazichukuliaje wewe binafsi katika kuendelea kutimiza zile ndoto zako? Kama huna hali moja wapo kati ya hizo je unapokutana nazo ghafla katika safari yako ya maisha ya hapa dunia upo tayari kukabiliana nayo au itakupotezea kabisa morali ya kuendelea kuishi hapa duniani na utamani kufa kabisa! Kwa nchi yetu ama kwa desturi nyingi imeonekana kuwa mtu akiwa kilema ni mtu wa kuombaomba pesa kidogo na misaada mingine ya kusukuma maisha yake, sikatai na wala siwezi pingana na hili lisitokee bali nataka nikufikirishe tofauti kuhusu kujiletea mafanikio makubwa ukiwa na hali hiyohiyo ya ulemavu. Najifunza mambo makubwa sana kwa Nick huyu ni mtu asiye na mikono wala miguu zaidi ana kipisi tu cha mguu si mguu na wala si mkono huwa nashindwa kuelezea vizuri maana huna mwonekano wa mguu wala huna mwonekano wa mkono ila upo eneo la miguu inapokaa unaweza ukanisaidia, uliyeona video zake, pamoja na hayo yote amekuwa msaada mkubwa kwa watu waliokata tamaa na ni mtu mwenye mafanikio makubwa na anaifurahia hali yake jinsi alivyoumbwa hajawahi kukaa kufikiri kuwa omba omba, hajawahi kukaa kufikiri kwa nini Mungu aliniumba sina viungo vyote, hajawahi kujiona hafai japo naamini kabla ya kujitambua alikuwa anajiona hafai kama wewe unavyojiona sasa hivi hufai kwa sababu umefeli masomo, umejiona hufai kwa sababu umeanguka kwenye biashara yako, umejiona hufai kwa sababu ulioa/kuolewa ikatokea bahati mbaya ndoa yenu ikaleta shida ikapelekea mkaachana, hapo nyuma ulikuwa mtu mkubwa katika jamii ila ikatokea ukarudi nyuma kwa kukosea sehemu sasa watu hawakuheshimu tena na wamekutoa eneo walilokuweka, familia yako imeyumba sababu hauna kipato tena cha kukuingizia pesa, kila ukiwaza unaona dunia yote inakucheka/kukuzomea wewe.
SOMA; USHAURI; Kuanza Biashara Kwa Mtaji Kidogo, Mambo Muhimu Ya Kuzingatia Ili Kuikuza.
Ufanyeje sasa unapojikuta kwenye hali hizi? kwanza kubaliana na jinsi ulivyo kwa sasa, furahia jinsi Mungu alivyoruhusu upatwe na hilo baya mpaka kupelekea kuwa hivyo maana hakuna anayejua hivyo viungo ulivyovipoteza vingekukosesha nini zaidi ya kukuharibia maisha yako ya kimwili na kiroho, kama umezaliwa huna miguu/mikono huo ni mpango wa Mungu jua unacho kitu cha kufanya kuleta maajabu ya dunia acha kujikunyata, acha lawama, acha kujiona wewe ni maskini, kutokubali hayo madhaifu una ruhusu akili yako kufanya kazi zaidi, una ruhusu watu kuona kile kitu cha ziada ulichonacho ndani mwako, na kama hukuzaliwa hivyo ila ikatokea kuna kosa ulifanya hapo nyuma kukupelekea kuwa hivyo ulivyo jisamehe kabisa, unapojisamehe una ruhusu moyo wako kuwa na ujasiri wa kufufua kile kitu kilichowekwa ndani mwako vinginevyo utajiona mtu usiye na faida na hicho Mungu alicholiweka ndani mwako utakufa nacho bila kujua ulikuwa na nini na watu hawataona umhimu wako wa kuja dunia, usikubali kuzikwa na hazina yako bila manufaa yeyote.
SOMA; Mambo Nane(8) Yatakayokufanya Uwe Na Fikra Chanya Kila Wakati Ili Uweze Kufikia Mafanikio.
Tumia hali uliyonayo kujiletea mafanikio, ukiwa na sauti ya kwanza halafu wewe ni mwanaume na una kipaji cha kuimba, imba haswa mpaka uone hapa nimeimba, huna mikono wala miguu ila una uwezo wa kuongea simama mbele za watu kuwafariji maana kuna watu wamekata tamaa na hawaoni tena mbele, raha iliyoje wewe ndio ukawa sehemu yao ya kujitambua? raha iliyoje kama hii makala ndio inaenda kuwa mwanzo wako wa kuinuka  tena? Raha iliyoje ukiwa una maumivu ya muda mrefu ila sasa unaenda kuagana nayo… hii ni furaha kubwa kwa wale wanaofanya vile vitu ambavyo wanavifurahia na wamevikubali ndani mwao, haijalishi mwanzo wao ulikuwaje hapo nyuma, wakati ni sasa usiangalie nyuma.
Nikutakie wakati mwema na mwanzo mpya wa maisha yako, ni mimi rafiki yako anayependa uwe na furaha na amani.
Waweza wasiliana nami Samson Ernest, kwa email; samsonaron0@gmail.com, whatsApp 0759808081 pia waweza tembelea www.mtazamowamaisha.blogspot.com
Asante sana.

2 thoughts on “Jinsi Ulivyo Unajikubali Katika Kujiletea Mafanikio Makubwa?

Add yours

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: