Hiki ni kitabu kinachotoa mbinu na maarifa ya kuweka kupangilia vitu vyako vizuri.
Ukweli ni kwamba kila mmoja wetu ana vitu vingi zaidi ya anavyohitaji. Lakini linapokuja swala la kuachana na vitu hivyo, iwe ni kwa kutupa au kwa kugawa inakuwa vigumu sana.
Kupitia kitabu hiki unajifunza mbinu za kufanya hili kwa urahisi na bila kuumia moyoni.
1. Kama vitu vyako haviko kwenye mpangilio mzuri basi akili yako nayo inakuwa haipo kwenye mpangilio mzuri kitu ambacho kinapelekea maisha yako pia kukosa mpangilio mzuri,
2. unapoiweka nyumba yako kwneye mpangilio mzuri, unaweka mahusiano yako na jana yako kwneye mpangilio mzuri pia. na hapa unapata nafasi nzuri ya kuona ni nini hasa unachotaka kwenye maisha yako. kwa kuwa na mpangilio mzuri ni rahisi kuona nini hutakio na hivyo kuachana na kile ambacho hutaki.
3. huwezi kubadili tabia yako kama hutabadili jinsi unavyofikiri kwanza. na hili sio zoezi rahisi, kubadili fikra zako ni zoezi gumu ambalo linahitaji moyo kufanya. ni muhimu uweze kudhibiti mawazo yako kama kweli unataka mabadiliko kwenye maisha yako.
4. watu wengi wanaojaribu kuweka nyumba zao kwneye moangilio mzuri baada ya muda mfupi hukuta mpangilio huo umeshavurugika. hii ni kwa sababu hawatumii njia sahihi kupangilia nyumba zao. kujaribu kupunguza kitu kimoja kimoja inawez akuchukua muda mrefu. ila kama utachagua siku moja ya kuondoa vitu vyote ambavyo huhitaji, itakuletea ahueni kubwa.
5. ukiwa na nyumba au chumba ambacho hakijapangwa vizuri, kinaficha hisia zako nyingine za hofu au woga. lakini unapokuwa na chumba kimepangwa vizuri ni rahisi kujua hasa hisia hizo zinaletwa na nini badala ya kufikiri mpango mbaya wa nyumba au chumba ndio unakuletea hisia mbaya.
6. sababu moja watu wengi wanashindwa kupanga vitu vyao vizuri ni kwa kuwa hawajui hata ni vitu vingapi ambavyo wanamiliki. hivyo unakuta vitu vinazagaa tu bila ya kuwa na uhakika mtu anavitumia katika wakati gani.
7. kuweka vitu vyako kwneye mpangilio mzuri kunahusisha mazoezi mawili muhimu.
zoezi la kwanza ni kutupa, na hapa unatupa chochote ambacho huna matumizi nacho.
zoezi la pili ni kuamua kitu fulani kikae wapi. hapa inakuwa rahisi kwako kujua kitu unachotaka kinapatikana wapi.
8. moja ya faida kubwa ya kutupa au kugawa vitu ambavyo hutumii ni kujiona upo huru na hakuna kinachokushikilia. wengi wetu tuna vitu vingi vinatushikilia kiasi cha kufikiri kwamba hatuwezi kuendelea na maisha kama tunakosa kitu fulani. Lakini tunapoachana nacho na maisha yakaendelea inatupa uhuru mkubwa.
9. kuzuia kukusanya vitu tena baadaya kuwa na mpangilio mzuri wa vitu, hakikisha unapoamua kuachana na vitu unafanya hivyo haraka na unafanya mara moja. na ukishaamua kitu fulani kinaondoka kiondoke kweli
10. ni kigezo gani utumie kuondokana na vitu usivyohitaji na kuwa na mpangilio mzuri?
kumekuwa na vigezo vingi watu wamekuwa wanatumia.
kama hujatumia kitu kw amwaka mzima, hukihitaji tena.
kama kitu kimeharibika na hakiwezi kutengenezeka ni kuachana nacho.
kitu ambacho kimepitwa na wakati pia.
11. njia bora kabisa ya kujua ni kitu gani uachane nacho au ubaki nacho, shika kitu hiko kwenye mikono yako na jiulize je kinakuletea furaha. kama jibu ni ndio, endelea kuwa nacho, kama jibu ni hapana, weka mbali mara moja na achana nacho(tupa au gawa).
12. chagua vile vitu mabavyo vinakupa furaha na baki navyo. na kama kigezo hiki bado kinakupa shida, yaani unaona kama kila kitu kinakupa furaha basi tumia vigezo vingine kama hisia ulizonazo juu yakitu hiko, matumizi yake, au taarifa muhimu kuhusu kitu hiko.
13. unapochagua kutupa au kugawa baadhi ya vitu vyako, hakikisha familia yako hawakuoni wakati unafanya bzoezi hili. kwa sababu watakurudisha nyuma. unaweza kusema unatupa au kugawa nguo ambazo hujatumia, akatokea ndugu yako akakuambia hii usitoe nitaivaa mimi, ukampa na bado asiivae. wengi wamekuwa wanakusanya vitu kwa njia hii, hata kama hawana uhitaji.
14. njia nzuri ya kumsaidia mtu na kitu unachotaka kutupa au kugawa ni kumuuliza kama kuna kitu chochote muhimu kwake ambacho amepanga kununua kwa siku za karibuni. kama kitu hiko kipo kati ya vile unavyotaka kutoa mpatie. ila kama hakipo, safisha vitu vyako kimya kimya.
15. kama wewe unapend akupanga vitu vizuri lakini wengine kwenye familia wanavuruga au kupanga vibaya, usiumie wala kuwalazimisha. wewe tumia muda wako kupanga vizuri na baada ya muda utawaona na wao wakijifunza kupanga vizuri. ila ukikazana kuwapangia vitu vyao watakuona wewe ni mbaya.
16. kwa wale ambao wana wadogo zao, wamekuwa wakijikuta wanawaachia mizigo ya nguo ambazo hata hawawezi kuvaa. au kama wewe umekuwa na wakubwa zako, umekuwa unaachiwa nguo nyingi sana. Hii inakupamzigo kwa sababu nguo za kupewa huwezi kutupa au kugawa, hii ni imani ambayo wengi tumejijengea. Ila kwa sasa kama nguo huivai na haikupi furaha basi tupa au gawa.
17. sio kila mtu utakayekutana naye kwenye maisha yako atakuwa rafiki yako. hivyo pia kwenye vitu unavyomiliki, sio kila kitu utakachonunua utakipenda kweli. hivyo usione uzito kuachana na vile vitu ambavyo huna matumizi makubwa navyo.
18. ili uweze kufurahia vitu vipya ulivyo navyo, ni lazima kwanza utupe vile vya zamani ambavyo kwa sasa huvitumii. kwa kuwa na rundo la vitu kunakufanya usione umuhimu mkubwa wa vile vipya ambavyo unavyo kwa sasa.
19. vitabu ni moja ya vitu vigumu sana kwa watu kuachana navyo. watu wengi hujikuta wana vitabu vingi wakifikiri kuna siku watahitaji kuvisoma tena. ukweli ni kwamba ni vitabu vichache sana ambavyo utahitaji kurudia kusoma. ukishasoma kitabu tayari umeshapata yale maarifa ya kile kitabu, iwe unakumbuka au la. songa mbele kwa kutafuta vitabu vingine vizuri zaidi.
20. kuwa na vitabu vichache kunaongeza nafasi yako ya kuvisoma. inakuwa rahisi kujua ndani ya kitabu fulani utapata maarifa fulani. lakini unavyokuwa na vitabu vingi unawez akujikuta unababaika kwa kila kitabu.
21. kama kuna karatasi yoyote ambayo huna matumizi nayo tena tupa. kama umeenda kutoa hela atm na ukatoa risiti, hakuna maana ya kuw ana risiti nyingi kwa wakati mmoja, kama unayo ya zamani, tupa pale unapochukua risiti mpya.
Jifunze na yatumia hayo uliyojifunza kwenye maisha yako.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani.