Kitabu THE LUNCH TIME TRADER ni kitabu kinachofundisha jinsi ya kufaidika na uwekezaji kwenye soko la hisa. Kupitia kitabu hiki unajifunza mbinu za kununua na kuuza hisa ili kuweza kupata faida kubwa.
Kuna mengi mazuri kwenye kitabu hiki, ila hapa nitakushirikisha sababu 20 kwa nini uwekeze kwenye kununua hisa.
SABABU 20 KWA NINI KILA MTU AWEKEZE KWENYE SOKO LA HISA.
Kama mpaka sasa hujawekeza kwneye soko la hisa unajinyima faida kubwa sana na nafasi ya kufikia uhuru wa kifedha, zifuatazo ni sababu 20 kwa nini uwekeze kwneye soko la hisa;
1. Unamiliki kampuni bila ya kufanya kazi au kujishughulisha na chochote. Wewe unawekeza fedha yako na yenyewe inakufanyia kazi na kukuingizia faida wakati wewe unaendelea na mambo yako mengine. Na hata kama umeajiriwa unaweza kuendela na ajira yako bila ya kuhofu kuhusu mambo ya fedha baadae.
2. Ni uwekezaji huru kwa wote. Uwekezaji kwenye soko la hisa haijalishi una miaka mingapi, ni kabila gani, jinsia wala tofauti yoyote ile. Ukishakuwa na fedha tu kidogo ya kununua hisa basi soko la hisa lipo wazi kwako na unaweza kuwekeza.
3. Unaweza kuanza na mtaji kidogo sana ukilinganisha na kuwekeza kwenye biashara nyingine. Kwa fedha kidogo sana unaweza kuingia kwenye uwekezaji wa kununua hisa.
Kwa Tanzania unaweza kuanza kwa tsh elfu 20 tu, na ukaendelea kuwekeza kufikia uhuru wako wa kifedha.
4. Uwekezaji huu unakupa uhuru mkubwa sana wa muda wako. Huhitaji kuwepo kwneye biashara unayowekeza, huhusiki na majukumu ya kila siku, unaweza kusafiri kwenda utakapo lakini uwekezaji wako unaendelea kukuzalishia.
5. Uwekezaji huu unakupa uhuru wa eneo. Huhitaji kuwa eneo fulani ndio uwekeze. Kwa mfano kwa Tanzania, japo hisa zitanunuliwa dar es salaam, huhitaji kuwepo dar ndio uweze kuwekeza. Unaweza kuwa popote tanzania na kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano ukanunua hisa zako.
6.  Huhitaji elimu kubwa ili uweze kuingia kwneye uwekezaji huu. Huhitaji kuwa na shahada yoyote ndio uweze kuwa na sifa ya kuwekeza. Kama unajua tu kuhesabu fedha na kujua faida na hasara basi unayo nafasi ya kuwekeza kwenye soko la hisa. Japo utahitaji kujifunza wewe mwenyewe zaidi kuhusu uwekezaji, au ukapata washauri wazuri.
[20:07, 9/12/2015] Makirita Amani: 7. Ni uwekezaji wenye uhakika wa kuendelea kuwepo miaka mingi ijayo. Haitakuja kutokea kwamba itanganwe soko la hisa limefutwa. Tofauti na biashara nyingine ambazo zinaweza kuingiliwa na mipango ya kiserikali.
8. Hakuna ushindani wa kibiashara kwenye uwekezaji wa hisa. Na uzuri ni kwmaba kadiri watu wengi wanavyoingia kwneye uwekezaji, ndivyonunavyozidi kupata faida. Hivyo wakinunua wengi bei inapanda na  unaweza kuuza kwa faida. Wakiuza wengi bei inashuka na unaweza kununua na ukaja kuuz akw afaida. Kikubwa ni uwe na maarifa.
9. Uwekezaji huu hauingiliwi na anguko la uchumi. Uchumi unaposhuka, wawekezaji wenye akili ndio wanazidi kupata faida. Wakati wengine wanapanic na kuuza wao wananunua, baadae soko likirudi vizuri wanaanza kuuza kwa bei juu.
10. Huhitaji kununua vitu au kufanya mahesabu ya stock, wewe ni kujua tu ni hisa kiasi gani unamiliki na soko linaendaje. Mengine hayo yatafanywa na kampuni unazowekeza. Yaani kwa kifupi wewe ni bosi mkubwa. Unapewa tu taarifa.
11. Huingii gharama kubwa kama kuendesha biashara. Gharama pekee unazoingia na kulipa madalali wa soko la hisa, baada ya hapo unaendelea na uwekezaji, kampuni zikipata faida na wewe unapata faida.
12. Huhitaji kwenda kukopa fedha ndio uingie kwenye uwekezaji huu, kama ilivyo kwenye biashara na ujenzi. Hapa unaweza kuanza na fedha kidogo uliyonayo na ukaendele akuongeza kila mwezi.
13. Hakuna vikao. Kitu kikubwa kinachopoteza muda kwenye biashara na kazi kama vikao. Ukiwekeza kwenye hisa unaokoa muda wako na utahudhuria vikao vichache sana vya wanahisa mwishoni mwa mwaka.
14. Hutafanya kazi yoyote ya kutumia nguvu. Yaani ukiwekeza kwneye hisa, wewe unaweza kulala kabisa kwa sababu huhitaji kugusa kitu chochote. Ni maarifa yako tu ya kuchagua kampuni nzuri za kuwekeza na unatengeneza kipato, ukiwa hata umelala.
15. Unaweza kuondoka kwneye uwekezaji huu muda wowote na kwa haraka sana. Ukiamua kwmaba hutaki tena unauza hisa zako na unapewa fedha yako. Tofauti na uwekezaji mwingine ambao huwezi kuondoka haraka hivyo.
16. Una nafasi kubwa ya kupata faida kubwa sana. Ukiwa na maarifa ya kuweza kuchagua makampuni mazuri ya kununua hisa, unawez akupata faida kubwa sana kama gawio na hata kuja kuuza hisa ambazo zinakuwa zimeongezeka thamani.
17. Uwekezaji huu unakupatia kipato ambacho hakina kikomo. Tofauti na uwekezaji mwingine au ajra ambapo kipato chako kinaamuliwa, kwenye uwekezaji wa hisa kipato kinaweza kuongezaka mara dufu na wewe unaweza kupata bila ya kuzuiwa.
18. Unaweza kuwafundisha watoto wako na wao wakanufaika sana baadae. Na kadiri watakavyoanza wakiwa wadogo, ndivyo wanakuwa kwneye nafasi nzuri sana ya kufanikiwa kupitia uwekezaji kwenye hisa.
19. Unabadili mtazamo wako kuhusu fedha na unaacha kuona kuna uhaba wa fedha na badala yako unaona zipo nyingi na hivyo kuzudi kuzivutia zaidi. Na pia unaweza kupiama maendeleo ya uwekezaji wako kwa haraka zaidi.
20. Kadiri unavyopata maarifa ndivyo kipato chako kinavyoongezeka. Jinsi unavyojifunza kuhusu uwekezaji wa hisa na jinsi unavyoweza kuchagua kampuni nzuri za kuwekeza ndivyo unavyozidi kunufaika.
Kazi ni kwako sasa, unasubiri nini usiwekeze kwenye hisa?
ANGALIZO; Kuwekeza kwneye hisa pia unaweza kupata hasara, lakini ukiwa na maarifa sahihi utapunguza sana nafasi za wewe kupata hasara.
Kila la kheri.