Kama unavyojua mpaka sasa, mafanikio hayatakuja kwa wewe kufanya vitu vya kawaida na kwa njia za kawaida.
Mafanikio yatakuja kwa wewe kufanya kazi kwa juhudi na maarifa. Kwa kifupi ni kufanya kazi sana, sio kidogo.
Na lazima uwe tayari kwenda hatua ya ziada, kwenda zaidi ya wengine walivyozoea kwenda, kutoa zaidi ya watu wanachotegemea kupokea.
Hapo ndipo mafanikio makubwa unayotaka unavyoweza kuyafikia.
Lakini….
Inabidi kazi hii kubwa unayofanya uwe unaipenda kweli, iwe inatoka ndani ya moyo wako. Pale wenzako wanapoondoka kazini saa kumi na kwenda kupumzika, na wewe kaamua kubaki masaa mawili ya ziada uwe kweli unabaki kutoka ndani ya moyo kwao na sio unafikiri kwamba na wewe ungekuwa umepumzika.
Pale wafanyabiashara wenzako wanapofanya biashara zao kwa mazoea kwa sababu wateja nao wamezoea hivyo, na wewe kuamua kubadili, japo wateja bado hawajaozea, iwe kweli umedhamiria kufanya hivyo na sio kufanya huku ukifikiri mbona wengine wanafanya kawaida na maisha yanaenda.
SOMA; Kama Una Tabia Hizi 30 Tayari Wewe Ni Mjasiriamali, Chukua Hatua.
Unaweza kufanya kazi kubwa, na kuifanya kwa juhudi kubwa na maarifa, kama tu hii inatoka kweli ndani ya nafsi yako. kama ndio kitu unachopenda sana. Kama ndio kitu unachoamini unaweza kufanya bora na kuwasaidia wengine wengi.
Swali ni je umeshapata kitu cha aina hii?
TAMKO LANGU;
Najua naweza kuweka juhudi kubwa na maarifa kwenye kitu ambacho nakipenda kweli, kwenye kitu ambacho kinatoka ndani ya moyo wangu. Mimi ninachopenda kweli kufanya ni hiki……..(jaza hapo). Nitaweka juhudi zangu zote, nitaweka maarifa yangu yote mpaka nihakikishe naleta mabadiliko makubwa kwangu na kwa wengine kupitia kitu hiki.
NENO LA LEO.
Do what you love to do and give it your very best. Whether it’s business or baseball, or the theater, or any field. If you don’t love what you’re doing and you can’t give it your best, get out of it. Life is too short. You’ll be an old man before you know it.
Al Lopez
Fanya kile unachopenda kufanya, na kifanye kwa ubora wa hali ya juu. Iwe ni biashara, michezo au kingine chochote. Kama hupendi unachofanya, na huwezi kukifanya kwa ubora wa hali ya juu, achana nachi. Maisha ni mafupi sana. Utajikuta umeshazeeka bila ya wewe mwenyewe kujua.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
TUPO PAMOJA.
