Mteja Wako Hahitaji Mikakati yako, Anahitaji Huduma Bora.

Habari za leo mpenzi msomaji wa makala za AMKA MTANZANIA. Bado unaendelea kuweka juhudi zako kwa yale uliyopanga mwaka huu au umeshakata tamaa?
Usijaribu kufanya hivyo, kazana hata kama unaona matokeo yake ni madogo. Cha kuzingatia ni kusogea hatua moja kwenda nyingine, haijalishi ni ndogo kiasi gani.

Wengi wetu tunatamani kuanzisha biashara, na wengi tulianza tukaishia njiani. Na wachache wetu hatuna matumaini ya kuendelea mbele, na wanahesabika waliofanikiwa.
Tunashuhudia zile kampuni/mashirika makubwa yalianza na moto na kasi kubwa, ila leo hii yamepoa na mengine yamekufa. Ukifuatilia sana chanzo cha mteja kuacha kutumia bidhaa zao. Ni kwamba mteja alipata tatizo akashindwa kupata msaada, na maelezo ya kwa nini lilimtokea tatizo hilo, hakupata.

MFANYE MTEJA AJISIKIE VIZURI KUFANYA BIASHARA NA WEWE.


Mteja anapokosa msaada wa uhakika wakati alinunua bidhaa yako. Unatengeneza sumu mbaya sana ndani ya fahamu zake, na hiyo sumu ataisambaza kwa wateja wengine zaidi. Hata kama anayeambiwa hakupatwa na tatizo hilo, kama anayemwambia atamwamini, tayari utakuwa umempoteza na huyo.

SOMA; Sababu Tano (5) Kubwa Kwa Nini Biashara Nyingi Hazifanyi Vizuri
Maneno yana nguvu sana kukuza biashara yako, na maneno yana nguvu sana kubomoa/kuharibu biashara yako. Unaweza ukakazana sana kutangaza biashara yako kwenye vyombo vya habari, ama kubandika bango zako maeneo mbalimbali. Kama unatoa huduma mbovu, mteja atapata taarifa kabla hata hajafika kwako.

Haya yote husababishwa na nini?

Wafanyakazi wako; unaweza ukakazana kutoa bidhaa zenye kiwango cha ubora wa Hali ya juu, ila ukakwamishwa na mfanyakazi wako. Mteja anapata kauli mbovu, mteja anakutana na dharau, mteja ana shida inayohitaji msaada wa haraka, anayemhudumia haonyeshi kumjali.
Mteja mwingine amekutana na sifa ya bidhaa zako kwa marafiki zake, anafika kwako anakutana na vitu viwili tofauti. Sababu nini, sababu maelezo aliyoyapata yamepishana na jinsi alivyotarajia kwenye uhalisia.
Anakutana na kauli mbili/tatu tofauti. Na zote kila mmoja alionyesha kujua, hii kwa mteja makini anapata wasiwasi na kuona hapa kuna ubabaishaji.

Wapo wateja waliowahi kuumizwa kwa hasara walizopata kwenye huduma yako. Unapokutana na mteja wa namna hii lazima ujue namna ya kuongea naye.
Huwezi kuongea kama vile unamsomea ilani ya chama, lazima umsikilize yale machungu yake. Kisha uonyeshe kumsaidia, na kumwonyesha tatizo kama hilo halitampata tena.
Binadamu tunapenda kuonyeshwa tunasikilizwa tunapopata tatizo la kusababishwa/kujisababishia wenyewe. Pale tunapowaendea waliotukosea wakaonyesha kutojali, huongeza maumivu zaidi ya mwanzo. Ndio ilivyo pia kwa huduma zetu tunazotoa kwa wateja wetu, mteja anapopata tatizo halafu akakutana na maneno ya kutojali, unamwongezea picha mbaya kichwani mwake.

SOMA; Maswali Manne (4) Yakujiuliza Ili Uweze Kuongeza Ustawi Wa Biashara Yako.
Hakuna mtu anayependa hasara, wewe hupendi hasara, na mteja wako pia hapendi hasara. Sasa unapokutana na mteja amepata shida, na akaja kwako, mpe nafasi ya kuongea. Usimwonyeshe kuwa anachokiongea ni upuuzi, usimkate ghafla katikati ya mazungumzo yake. Subiri Akishatulia, anza kumwelezea taratibu, ongea naye kama vile unaongea na mtu ambaye ndio kwanza anaijua biashara yako. Usimburuze na maneno, ongea kwa kumaanisha kile kilichomfanya asifurahie kile alichokinunua kwako.
Ukiwa na tabia hii, mteja hata kama alikuja kwa nia ya kutaka kitu chake kirudi na wewe unajua hakuna uwezekano wa kukirudisha. Utashangaa kwa huduma uliyompa, anakuwa rafiki yako mkubwa maana amepata ufumbuzi wa tatizo lake.

Kauli zako kwa mteja, zinaweza kujenga msingi imara wa biashara yako. Mteja anapokuletea mashitaka kama wewe ni boss, kwa huduma mbaya aliyoipata kwa mfanyakazi wako, usipende kupuuzia. Iwe ina ukweli ama haina ukweli, jaribu kuipima kwa kuongea naye.
Kumbuka mteja anahitaji huduma na si sera zako, kilichokuunganisha wewe na mteja ni bidhaa zako. Huyo tayari ni rafiki yako, mjenge zaidi aendelee kuwa rafiki ambaye atakuchukulia madhaifu yako yanapojitokeza bila kutegemea.
Hizo ndio huduma bora kwa mteja, na si bora huduma, na si maneno tu.
Kuna kitu umejifunza? kama ni ndio, kifanyie kazi.

Makala hii imeandikwa na rafiki yako;
Samson Ernest ~
0759808081/0715591559.
Email:
samsonaron0@gmail.com
Blog: www.mtazamowamaisha.blogspot.com

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: