Dunia sio mapambano ya kupata au kukosa.

Sio kweli kwamba kuna uhaba kama tunavyoaminishwa.

Sio kweli kwamba ili wewe uwe tajiri ni lazima wengine wawe masikini.

Chochote unachotaka, kipo cha kukutosha wewe na wengine wengi wanaokitaka pia.

ZIPO FURSA ZA KUMTOSHA KILA MTU.
ZIPO FURSA ZA KUMTOSHA KILA MTU.

Unapoiruhusu akili yako kuwafikiria wengine pia, unairuhusu kufikiri kwa ukubwa zaidi, unaimarisha ushirikiano zaidi na unapata zaidi.

Unapoipa akili yako hali ya ubinafsi, ya kupata wewe tu, ya kuchukua kutoka kwa wengine, unaondoa ushirikiano na pale ambapo hakuna ushirikiano, hakuna mafanikio.

Chochote unachotaka, taka na wengine pia nao wakipate.

Fursa zipo nyingi za kumtosha kila mmoja wetu. Tushirikiane.

SOMA; Unataka Kuwazidi Wengine? Umeshapotea.

TAMKO LANGU;

Najua ya kwamba fursa zipo nyingi sana za kunitosha mimi na wale wote wanaonizunguka. Chochote ninachotaka nitataka na wengine nao pia wakipate. Kwa njia hii nitaimarisha ushirikiano na ushirikiano huu ndio utaniletea mafanikio makubwa.

NENO LA LEO.

What I want for myself I want for everyone

Samuel Milton “Golden Rule” Jones

Chochote ninachotaka mimi, nataka kila mtu pia akipate.

Rafiki na Kocha Wako,

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

TUPO PAMOJA.