Wote tunajua kusema ni rahisi kuliko kufanya, hiyo sio habari.
Habari ni hii, kuna watu wanasema na wanafanya, ila changamoto inaanzia hapa, wanachosema wanafanya sio kile wanachokwenda kufanya.
Wanasema hiki na wanafanya kingine.
Kwa kuanzia fikiri kila mtu anakwenda kufanya tofauti na kile anachosema atafanya, halafu angalia ni jinsi gani unaweza kushawishi afanye kile ambacho kweli amesema atafanya.
Bila ya wewe kuweka ushawishi ni vigumu sana kwa mtu mwenyewe kufanya kile alichosema atafanya.
Na elewa hapo nimesema ushawishi na sio nguvu, maana utakapoweka nguvu utamfanya atake kufanya hovyo zaidi.
Kuamini tu mtu anaposema na wewe ukaenda na yako, unatoa nafasi ya kuangushwa au kuumizwa.
Hali hii ipo kwenye kila eneo la maisha ambapo mtu mwingine anakuahidi wewe kufanya kitu.
SOMA; UAMINIFU; Jinsi ya kujijengea tabia ya uaminifu.
TAMKO LANGU;
Najua ya kwamba kile watu wanachosema watafanya sio wanachokwenda kufanya kweli. Ili kuzuia hili kwa yale mambo ambayo ni muhimu kwangu, nitahakikisha nina ushawishi kwa yule mtu ambaye ameniahidi kufanya kitu fulani ili aweze kukifanya kweli.
NENO LA LEO.
Between saying and doing, many a pair of shoes is worn out.
Iris Murdoch
Katikati ya kusema mpaka kufanya, viatu vingi sana vinaisha.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
TUPO PAMOJA.