Je Unachotaka Kufanya Umekubaliana Nacho Ndani Yako? Soma Hapa Kujua Zaidi.

Habari za leo rafiki, vipi unaionaje Amka Mtanzania katika kubadili maisha yako. Kama kuna kitu unakipata au umekipata kupitia mtandao huu, usiache kuwa shuhuda kwa wengine. Hii itasaidia kujenga kizazi bora zaidi jinsi siku zinavyoenda mbele, kuwa miongoni mwa watu waliobadilisha maisha ya wengine waliokata tamaa.


Usikae kimya kwa vile vitu vizuri unavyovipata humu, umepata bure na wewe toa bure.

Kuna mambo mengi huwa tunatamani kuyafanya katika maisha yetu. Ila inapofika katika matendo huwa tunakata tamaa mapema mno kabla ya kufikia lengo lile tulilolikusudia.
Hakuna anayependa hali hii, ila hutokea katikati ya safari yetu. Ubaya zaidi matatizo mengi hayafanani kutoka na kile ulichokuwa unakitaka wewe. Hii ikiwa na maana kwamba, kuna ambaye alitamani kuwa mfanyabiashara, akaanza kufanya hiyo biashara. Na kuna mwingine alitamani kusoma, hawa watu wawili changamoto zao haziwezi kufanana wala kulingana, japo wote wanapitia wakati wa kushindwa.

SOMA; Hii Ndio Changamoto Kubwa Inayokuzuia Wewe Kutatua Changamoto Zako.
Unachotakiwa kujua siku zote ni kwamba, chochote unachotaka kufanya kina changamoto yake, chochote unachofanya kina changamoto yake, hatua yeyote unayopitia au unayotaka kuianza, ina changamoto yake. Ukilijua hili hutokaa upate shida kamwe katikati ya safari yako.
Hii pia haiwezi kutosha kama hutofanya uchunguzi wako wa ndani ya nafsi yako, yaani uridhie kile unachotaka kufanya.

Urahisi wa kupenya kitu unachokihitaji, hata ukitokea ugumu wa kutengwa na watu wako wa karibu kwa kile ulichokiamini, na chenye kibali ndani ya moyo wako, ni kuhakikisha ndani yako umejipanga na umekubali kubaliana na hilo jambo, kwa hali yoyote itakayojitokeza.
Kulipokea jambo kwa hamasa na kulifikiria kwa undani, ukapata muda pia wa kujifunza kuhusu hilo unalolihitaji. Inakupa ujasiri zaidi wa kupenya popote pale inapoonekana kuna ugumu wa kupita.

Hapa tutaona wengi wetu tumeshindwa kwa sababu, tuliendeshwa na hisia tu za kuona wengine wakifanikiwa kwa hilo jambo pasipo kujua gharama yake. Laiti tungekuwa tunapata muda wa kutafakari, na kupata muda wa kukaa na wale wanaoshughulika na hilo jambo tunalolihitaji tungekuwa mbali sana.
Laiti tungekuwa haturidhiki na mafanikio machache tunayopata, zaidi tungejikita zaidi kwa wale waliofanikiwa tukapata muda wa kusoma vitabu vyao, tukasikiliza audio zao na kuangalia video zao, umbali wa kufikia malengo yetu usingeonekana pale tunapokutana na changamoto.

Mazoezi makubwa tunayotakiwa kuyafanya katika kufikia mafanikio makubwa ya malengo yetu kwa kile tunachotaka kufanya au tulichokianzisha kukifanya. Lazima tufanye makubaliano sisi wenyewe ndani ya fikra zetu, vinginevyo tutaendelea kushindwa na kutafuta kisingizio cha kukubali kushindwa.
Katika kufikia safari yako ya mafanikio, kuna vikwazo vingi sana. Lazima uweke mipango yako vizuri isiyoharibika haraka kabla hujafanyia kazi, hakikisha kila mpango ulioupanga haukuponyoki mikononi hivi hivi pasipo kuutendea kazi kwanza.

SOMA; Hizi Ndizo Changamoto Kubwa Unazotakiwa Kuzivuka ili Kufikia UTAJIRI.
Jenga tabia ya kutokurupuka pasipo kutafakari mipango yako, jenga utulivu wa akili yako pale unapokwama njiani. Lazima upo mlango/njia ya kupita.
Jenga tabia ya kutojilaumu sana pale unapogundua umekosea, zaidi uwe wa kwanza kujisamehe. Hii huonyesha ulikubali kukinywea hicho kikombe, na itakuongezea hamasa ya kusonga mbele zaidi hata pale unapojihisi umechoka.

Utaratibu huu wa kufanya makubaliano wewe kwanza, ni utaratibu mzuri kwa yule anayehitaji kweli kupata kitu fulani. Usisahau hii ni mapatano ya wewe na serikali yako ya ndani kabisa, sisi tunaweza kukupa ushauri lakini wewe utabaki kuwa mwamuzi wa mwisho kufuata lipi na kuacha lipi.
Usikubali kuanzia leo kufanya kitu pasipo kufanya makubaliano yako ya ndani.

Asante kuwa pamoja nami.
Makala hii imeandikwa na rafiki yako Samson Ernest,
Blog;
www.mtazamowamaisha.blogspot.com
Email; samsonaron0@gmail.com
Mawasiliano; 0759808081.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: