Kwa hali ilivyo hakuna namna nyingine ya kulisema hili bali kusema kwamba umegoma kuishi.
Unapokazana kufanya mambo ambayo hayaendani kabisa na maisha, iwe unajua au hujui ni kwamba umegoma kuishi.
Unapokazana kusema kwamba maisha hayako sawa, maana yake umegoma kuishi, kwa sababu nani alikuahidi kuwa yatakuwa sawa?
Unapolalamika au kulaumu wengine kwamba ndio wanasababisha wewe maisha yako yanakuwa magumu maana yake umegoma kuishi, kwa sababu ni nani alikuahidi kwamba wengine wanatakiwa wakupe kile unachotaka?
Unapofanya vitu fulani ili uonekane, au unapofanya vitu kwa kuiga maana yake umegoma kuishi maisha yako ambayo yana maana kubwa kwako.
Unapoamua kukata tamaa kwa sababu umekutana na changamoto, umeamua wewe mwenyewe kugoma kuishi, kwa sababu ni maisha gani ambayo hayana changamoto?
Madhara ya kugoma kuishi.
Ni kukosa mafanikio, huwezi kupata mafanikio kama umegoma kuishi, mafanikio yanakuja kwa wale wanaoishi maisha yao.
Kabla hujalalamika kwamba huna mafanikio, au maisha yako ni magumu, jiulize je unaishi? Hili ni swali la msingi sana kabla hujaenda mbali zaidi.
TAMKO LANGU;
Najua ya kwamba nilikuwa nimegoma kuishi. Nilikataa kuchukua hatua ya kuendesha na kusimamia maisha yangu na kufikiri kwamba kuna mtu mwingine mwenye jukumu hilo. Sasa najua ya kwamba mafanikio yanakuja pale ambapo nitakapokua naishi maisha ambayo yana maana kwangu. Kuanzia sasa nimeamua kuishi maisha yangu.
NENO LA LEO.
People will always have an opinion, but you have to live life the way you want to. It’s very easy to tell others what to do, but difficult to implement it on yourself.
Preity Zinta
Watu mara zote wanakuwa na maoni, lakini wewe inabidi uishi maisha jinsi unavyotaka mwenyewe. Ni rahisi kuwaambia watu nini cha kufanya, lakini ni vigumu sana kutekeleza mwenyewe.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
TUPO PAMOJA.