Mambo 6 Yatakayokufanya Uzidi Kuwa Bora Na Mwenye Mafanikio Makubwa.

Habari rafiki na mpenzi msomaji wa AMKA MTANZANIA, naamini umzima afya na unaendelea na harakati za kuboresha maisha yako. Karibu tena katika siku nyingine ya kujifunza na kuboresha maisha yetu kama ilivyo kawaida yetu. Hili ni jukumu ambalo unatakiwa kuliendeleza karibu kila siku katika maisha yako.
Kumbuka, kama ambavyo tumekuwa tukisema mara kwa mara kupitia mtandao huu wa AMKA MTANZANIA  ni muhimu na ni lazima kuwa bora zaidi ili kujihakikishia mafanikio ya kudumu. Kwa wale wasomaji wazuri wa AMKA MTANZANIA wanalijua hili vizuri na umuhimu wa falsa ya kuwa bora kila siku katika maisha yetu.
Na katika kuhakikisha hili linafanikiwa huwa yapo mambo ambayo tunatakiwa tujifunze na kuyafanyia kazi kila siku. Mambo hayo, ambayo unatakiwa uyaelewe na kuyafanyia kazi ili uwe bora siku zote, baadhi tunakwenda kujifunza kupitia makala hii. Je, ni mambo gani yatakayokufanya uzidi kuwa bora na mafanikio makubwa?
Yafutayo Ni  Mambo 6 Yatakayokufanya Uzidi Kuwa Bora Na Mwenye Mafanikio Makubwa.
1. Jielewe mwenyewe.
Hatua mojawapo kubwa itakufanya uzidi kuwaa bora siki hadi siku ni wewe kujitambua kwanza. Kwa kujijua wewe itakusaidia kujua udhaifu wako na kuboresha yale maeneo ambayo kwako unaona yana shida au yana kukwamisha kwa kiasi fulani. Watu wengi huwa wanakwama au kuchelewa kufanikiwa kwa sababu ya kushindwa kujitambua wao mapema na yale mambo yanayo wakwamisha kufikia mafanikio hayo.
USHINDI NI LAZIMA UKIWA BORA SIKU ZOTE
2.  Kuwa na mawazo chanya.
Maisha yako yatakuwa bora zaidi na ya wepesi kama utakuwa mtu wa mawazo chanya. Kinyume cha hapo utageuza maisha yako kuwa mzigo mkubwa ambao utashindwa kuubeba. Hii ndiyo siri mojawapo pia ya kukufanya uzidi kuwa bora kwa kile unachokifanya. Hivyo, chochote unachokifanya kitazame kwa mtazamo chanya, hiyo itakusaidia kuwa bora sana.
3. Kuwa wewe kama wewe.
Utazidi kujihakikishia ubora mkubwa katika maisha yako ikiwa utabaki  kuwa wewe kama wewe. Hakuna mafanikio makubwa yanayoweza kupatikana kwa kuiga. Kumbuka umeumbwa ukiwa wewe kama wewe, hivyo kwa kila unalolifanya acha kuiga sana. Jifunze kuwa wewe kama wewe, kwani kuiga kuna mipaka yake. Ukifanikiwa kumudu hili itakusaidia sana kuwa bora kwenye maisha yako kuliko unavyofikiri.
4. Jiamini.
Siri kubwa ya mafanikio ipo kwenye kujiamini. Mipango na malengo mengi yanashindwa kufanikiwa kwa sababu ya kutokujiamini. Kwa kadri utakavyoweza kujenga nguvu kubwa ya kujiamini itakusaidia sana kuwa bora wakati wote na kuweza kufikia mafanikio makubwa ambayo unayahitaji katika maisha yako. Kwa kujiamini tu, itakusaidia kufikia mafanikio makubwa na kuwa bora zaidi kwenye maisha yako.
5. Kujifunza.
Hitaji la kwanza ambalo litafanya maisha yako yazidi kuwa bora ni kujisomea kila siku. Unatakiwa kujifunza kupitia vitabu, semina au mitandao ya kuhamsisha kama iliyo chini ya AMKA CONSULTANTS. Kwa bahati mbaya sana tatizo kubwa walilonalo watanzania wengi ni kule kushindwa kujisomea. Wengi hawapo tayari kupata maarifa haya. Kama wewe ni mtu wa kujisomea elewa utakuwa umeachana na kundi kubwa na kufuata njia ambayo itakupeleka kwenye  ubora siku hadi siku.
6. Kuwa msikilizaji mzuri.
Siku zote acha kuzungumza tu, kama unataka kuwa bora jifunze kuwa msikilizaji mzuri pia. Unapokuwa msikilizaji inakusaidia kujua mambo mengi ambayo hapo mwanzo hukuyajua kabisa. kumbuka hata watu wenye mafaniko ni wasikilizaji pia wazuri.
Yapo mambo mengi ambayo yanaweza kukufanya ukawa bora zaidi. Chukua hatua kwa kwa kuyafanyaia kazi hayo ili kufikia mafanikio  yako makubwa.
Endelea kutembelea AMKA MTANZANIA kila siku kwa ajili ya kujifunza.
Kwa makala nyingine nzuri pia tembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na kuhamasika.
 DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Simu; 0713 048 035,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: