Ni kupoteza muda wako na wa wengine pia.

Chochote unachoamua kufanya, kifanye kwa moyo mmoja, kifanye kwa juhudi zako zote na maarifa yako yote.

Au usikubali kabisa kukifanya, kwa sababu ambazo unaweza kuzitoa au usizitoe, amua ya kwamba hufanyi kitu hiko.

Kufanya kwa shingo upande, unaweza kuona unawasaidia wengine, lakini ukweli ni kwamba unawaharibia.

Kufanya kwa shingo upande unafanya kwa sababu tu inahitajika ufanye na hivyo huwezi kufanya kwa ubora wa hali ya juu.

Na kama huwezi kuwafanyia watu kitu cha ubora wa hali ya juu, unawanyima fursa ya kupata mtu mwingine wa kuwafanyia kitu vizuri.

Kufanya kwa shingo upande kunakuzuia wewe kupata fursa nyingine nyingi za baadae. Kwa sababu utafanya kitu kilicho chini ya viwango na kila atakayeona ulichofanya hatovutiwa kukutafuta ili ufanye na kwako.

Usifanye kitu chochote kwa shingo upande, usitake kufanya kitu ili kuwaridhisha watu fulani. Fanya kitu kwa sababu umejitoa kufanya na utaweka ubora wa hali ya juu sana.

SOMA; Sheri Namba Moja Ya WORLD CLASS; Fanya Zaidi Ya Unavyotegemewa.

TAMKO LANGU;

Nimejua kukubali kufanya kitu kwa shingo upande ni kupoteza muda wangu na wa wengine pia. Kuanzia sasa nitakubali kufanya kitu kwa moyo mmoja na nitaweka juhudi zangu zote, au nitakataa kufanya kile ambacho sio muhimu kwangu. Kufanya kwa shingo upande ni kujizuia mimi mwenyewe kupata fursa nzuri zaidi.

NENO LA LEO.

You can only do your best. That’s all you can do. And if it isn’t good enough, it isn’t good enough.

Imelda Staunton

Unachoweza kufanya ni kufanya kwa ubora. Hiko ndio pekee unachoweza kufanya. Na kama unachofanya sio kizuri, sio kizuri.

Usifanye kitu chochote kwa shingo upande, fanya kwa moyo mmoja na fanya kwa ubora.

Rafiki na Kocha Wako,

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

TUPO PAMOJA.