KITABU CHA FEBRUARI 2016; You Can Win (Unaweza Kushinda.)

Habari za wakati huu rafiki?
Ni wakati mwingine mzuri tena wa kwenda kupata kitabu kizuri cha kujisomea kwa mwezi huu wa pili. Kama ilivyo kwa utaratibu wetu, kila mwezi unatumiwa kitabu kizuri cha kujisomea ambacho kitakuongezea maarifa zaidi ya kukuwezesha kuwa na maisha bora na yenye mafanikio makubwa.

 
kwa mwezi huu wa pili tunakwenda kusoma kitabu YOU CAN WIN kitabu ambacho kwa tafsiri rahisi ya kiswahili kinakupa maarifa ya kushinda kwenye maisha yako. kwa kusoma kitabu hiki utapata mbinu za kushinda kwenye kazi, biashara na hata maisha kwa ujumla.
Kitabu hiki ni kizuri kwani kinaanza kuchimba ndani kabisa ambapo ni kwenye mtazamo wako. Nakukumbusha tena uko hapo ulipo kutokana na mtazamo ambao unao kwenye akili yako. yale mawazo yaliyokujaa ndiyo yanatengeneza maisha uliyonayo sasa.
Na kama unataka kutoka hapo ulipo, unahitaji kwanza kubadili mtazamo wako. Unahitaji kuwa na mawazo mapya ambayo yatakuletea mazingira bora kwako kuweza kufanikiwa.
Najua wengi tunapenda mabadiliko, lakini hatupendi kubadilika. Kupitia kitabu hiki utajifunza ni vitu gani vimekujengea mtizamo ulionao na jinsi gani unaweza kuubadili. Baada ya hapo ndio unaweza kuchukua hatua za kufikia ushindi mkubwa sana kwenye maisha yako ikiwa ni pamoja na kuweka juhudi kubwa sana kwenye kitu chochote unachoamua kufanya.
Rafiki yetu Daudi Mwakalinga aliandaa uchambuzi mzuri sana wa kitabu hiki. Kama bado hujasoma uchambuzi huo usome hapa; Mambo 20 Niliyojifunza Kwenye Kitabu Cha YOU CAN WIN (UNAWEZA KUSHINDA)

Pamoja na kusoma uchambuzi huo mzuri, tenga muda mwezi huu wa pili na ukisome kitabu chenyewe. Uzuri ni kwamba kitabu kinaeleweka kwani kimeandikwa kwa lugha rahisi kueleweka na pia ni kifupi. Hivyo kwa kusoma angalau sura moja kwa siku utajifunza mengi na kubadili maisha yako.
Pata kitabu hiki kwa KUBONYEZA MAANDISHI haya na utakipakua.
Soma na fanyia kazi yale utakayojifunza na maisha yako yatakuwa bora sana. Kumbuka kupata maarifa ambayo huyafanii kazi hutakuwa na tofauti na mtu ambaye hajapata maarifa kabisa. Na huenda yeye akawa na afadhali maana hakujua. Ila wewe uliyejua njia ya kuwa bora na hukuwa, utajilaumu maisha yako yote.
Usitake kujilaumu, jifunze sasa na chukua hatua.
Nakutakia kila la kheri katika usomaji wa vitabu.
TUPO PAMOJA.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani.
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s