Karibuni kwenye darasa letu la jumapili ya leo, ambapo tutakwenda kujifunza kuhusu MEDITATION (TAJUHUDI)
Kwenye darasa la leo tutashirikiana na Dr Bukaza Chachage ambaye pia ni mmoja wa watu wanaofanya meditation kila siku.
Kwa sehemu ya kwanza tutajifunza yafuatayo;
1. Maana ya meditatio,
2. Maandalizi ya kufanya meditation,
3. Jinsi ya kufanya meditation,
4. Muda wa kufanya meditation,
5. Faida za kufanya meditation.
Sehemu ya pili Dr Chachage atatushirikisha uzoefu wake wa kufanya meditation, jinsi anavyofanya na jinsi anavyonufaika nayo.
1. Maana ya MEDITATION (TAJUHUDI)
Meditation ni njia ya kuituliza akili na kuweza kuyadhibiti mawazo yako. Kupitia meditation unaweza kuyadhibiti mawazo yako na kuweza kuyapeleka pale unapotaka wewe (kufocus)
Kwa maisha yetu ya kawaida, akili yetu inakuwa na mawazo mengi sana katika wakati wowote ule.
Unakuwa unafikiria kazi au biashara zako,
Unafikiria kuhusu changamoto unazokutana nazo,
Unawaza makosa uliyofanya huko nyuma,
Una hofu ya mambo yatakayotokea,
Na mengine mengi.
Mawazo yote haya yanafanya mawazo yako yanaruka ruka kama nyani anavyorukia tawi moja la mti kutoka tawi jingine.
Hali hii inaleta uchofu na hata msongo wa mawazo.
Na pale unapotaka kutuliza akili yako chini ili ufanye kazi inayohitaji akili au ubunifu, unashindwa kufanya hivyo.
Sasa mawazo haya mengi yanakuja na madhara menhi kwetu,
Kushindwa kuconcentrate kwenye kitu kimoja na hili kupelekea kuwa na uzakishaji mdogo.
Kusababisha magonjwa ya moyo,
Kuchochea magonjwa kama saratani na kadhalika.
Hivyo kupitia meditation unaweza kuyatuliza mawazo yako, na kuweka umakini mkubwa kwenye kitu chochote unachofanya.
Pia unaweza kuondoa mawazo hasi yanayokuwa kwenye akili hako, ambayo yanachochea kuwa na mtazamo hasi.
2. Maandalizi ya kufanya meditation.
Meditation inahitajika kufanyika kwenye eneo tulivu hasa pale ambapo unaanza. Na pia inakuhitaji akili yako na mwili wako viwe vimepumzika (relax)
Hivyo kwenye maandalizi unahitaji kuzingatia yafuatayo;
2.1 eneo la kufanyia meditation.
Fanyia kwenye eneo ambalo hakuna usumbufu. Hivyo unaweza kuchagua kufanya muda ambao hakuna usumbufu kama unafanyia nyumbani au ofisini.
Unaweza kufanya asubuhi na mapema unapoamka na wengine wanakuwa bado hawajaamka.
Mazingira haya yanakuwezesha kufikia utulivu wa akili haraka zaidi.
2.2 mwili uwe umerelax.
Ili akili yako itulie, basi lazima mwili wako uwe umerelax hivyo usiwe na kitu ambacho kinaubugudhi mwili kama nguo zilizobana.
2.3 mkao wa kufanya meditatio.
Ili akili yako iweze kutulia, ni lazima mwili wako urelax na ili urelax unahitaji kuwa na mkao ambao hautaumiza mwili wako.
Kuna ambao wanapendelea kukaa kwa kukunja miguu, kama wanavyoswali waislamu.
Lakini siyo lazima ukae hivyo, unaweza kukaa kwenye kiti kawaida, au kwenye mkeka chini.
Muhimu mwili uwe vizuri ili usipate maumivu ambayo yatahamisha mawazo yako wakati unafanya meditation.
3. Jinsi ya kufanya MEDITATION.
Sasa hapa ndiyo kwenye shughuli yenyewe.
Kwa kuwa lengo la meditation ni kutuliza akili, na kwa kuwa akili yako muda wote inaruka ruka kwa mawazo mbalimbali, tunahitaji njia ya kuyatuliza mawazo haya.
Na njia hii ni kuhakikisha mawazo yako yote unayapeleka sehemu moja.
Sasa hapa kwenye kupeleka mawazo yako ndipo kunapoleta aina tofauti za meditation.
Hapa nitazungumzia aina mbili, ambazo ni nzuri na rahisi kuanzia.
3.1. Kupumua (BREATHING MEDITATION)
Kila mmoja wetu hapa anapumua, si ndiyo. Basi unaweza kutumia pumzi yako kama sehemu ya kufanya meditation.
Unachokifanya hapa ni kupeleka mawazo yako yote kwenye pumzi zako.
Unapoanza meditation, kaa sehemu yako ya kufanyia meditation, hakikisha umekaa vizuri kama tulivyoona kwenye maandalizi.
Funga macho yako, na anza kupumua.
Unapopumua peleka mawazo yako yote kwenye pumzi zako.
Na hapa kuna njia mbili;
3.1.1 fikiria pumzi yako tangu inaingia puani, ihisi inavyopita kwenye pua zako, kwenye koo lako mpaka kwenye mapafu yako na inavyotoka. Hisi kifua chako kinavyoinuka unapovuta pumzi na kinavyoshuka uapotoa pumzi.
3.1.2 hesabu pumzi zako. Hapa unahesabu moja unapovuta pumzi ndani, na mbili u apotoa nje, tatu ukivuta tena, nne ukitoa nje. Nenda hivyo mpaka kumi halafu anza tena.
Mambo muhimu ya kuzingatia hapo.
Utakapoanza zoezi hili mawazo yako yatakuwa yanahama hama, usijali, kama mawazo yameondoka kwenye pumzi na ukaanza kufikoria hofu zako, anza tena, siyo zoezi rahisi kudhibiti mawazo, lakini kadiri unavyokwenda utaona unaanza kuyadhibiti.
3.2 Kuangalia (VISUAL MEDITATION)
Aina nyingine ya meditation ni kuwa na kitu kimoja ambacho unakiangalia na mawazo yako yote unayapeleka pale.
Kwenye njia hii mawazo yako yanakuwa kwenye kile kitu ulichochagua kuangalia.
Na vitu vizuri kwa kuanzia ni mwanga wa mshumaa, au picha au kitu chochote akbacho kipo usawa wa macho yako.
Maandalizi ni yale yale ya kukaa vizuri na kisha macho yako yanalenga kitu kile. Angalia pale tu mpaka pale utakapokuwa huoni kitu kingine zaidi ya kile ulichochagua kuangalia.
Mawazo yako yatakuwa yanahama lakini yarudishe.
Kuna aina nyingine nyingi za meditation kama
Kurudia maneno fulani (mantra)
Kutembea (walking meditation)
Kwa kuanza nzuri ni KUPUMUA, ni rahisi na unaweza kudhibiti mawazo yako haraka.
4. Muda wa kufanya MEDITATION.
Kwenye muda hapa kuna mambo mawili ya kujifunza;
4.1 Muda unaotumia kufanya meditation.
Hapa chagua zoezi lako la meditation lichukue muda gani. Unaweza kufanya kwa dakika 5, dakika 10, dakika 20, nusu saa, saa moja na kuendelea.
Kwa kuanzia anza na muda wa chini, napendekeza dakika tano au kumi. Kama hizi zinakushinda anza hata na dakika tatu.
Kadiri unavyozoea na unavyoona manufaa yake unaweza kwenda muda mrefu zaidi.
4.2 Muda wa kufanya kwenye siku yako.
Ni vizuri ukachagua ni muda gani mzuri kwako kufanya meditation kwa siku. Muda mzuri ni mara baada ya kuamka, au baada ya kula, au muda wowote mzuri kwako kulingana na mazingira yako na kazi zako.
Pia unahitaji kufanya zaidi ya mawa moja kwa siku, angalau mara mbili au tatu.
Mimi huwa nafanya meditation kwa angalau dakika kumi kitu cha kwanza ni apoamka asubuhi. Na wakati mwingine kwenye siku yangu, kwenye chochote ninachokuwa nafanya. Nitakuambia zaidi hili.
Mwisho unaweza kuweka meditation kwenye kila unachofanya, na hii inaitwa MINDFULNESS, yaani kile unachochagua kufanya, unaweka mawazo yako yote pale.
Kama unakula chakula basi mawazo yako yote unayapeleka kwenye chakula kile, uipata kila ladha, kila unavyotafuna, kila unapomeza unakihisi kinavyoshuka.
Hivi unajua watu wengi huwa hatuli, tunajikuta tu tunameza chakula kwa haraka huku tukifikiria mambo mengine. Sasa unaweza kugeuza kitendo cha kula kuwa meditation yako.
Au kama unaendesha au umekaa kwenye chombo cha usafiri, unaweza kuchagua kuweka mawazo yako sehemu moja, usikimbilie kusoma gazeti, au kusikiliza wengine, bali mawazo yako unayaweka sehemu moja. Hili linahitaji uzoefu kidogo maana ni rahisi kusumbuliwa.
5. FAIDA ZA KUFANYA MEDITATION.
Zipo faida nyingi sana za kufanya meditation. Na tafiti nyingi za kisayansi na kitabibu zimeonesha watu wanaofanya meditation wanakuwa na afya bora ya akili na mwili.
Hizi hapa ni chache kati ya faida nyingi za meditation;
1. Inakuwezesha kupumzisha mwili na akili.
2. Inakuwezeaha kuondoa mawazo hasi kwenye akili yako.
3. Inakuwezesha kuondokana na msongo wa mawazo.
4. Inakuwezesha kuwa na uzalishaji mkubwa, kuweza kufanya mambo mengi kwa muda mfupi.
5. Inakuwezesha kurahisisha maisha yako. (Simplify)
6. Inakuwezesha kudhibiti hisia zako, vitu kama hasira havitakutawala.
7. Meditation inakuwezesha kuboresha kumbukumbu zako (memory)
8. Meditation inakuletea furaha na kuridhika na maisha.
9. Meditation inaboresha afya, kukuepusha na vidonda vya tumbo na magonjwa ya moyo.
10. Meditation inakuwezesha kufurahia chochote unachofanya.
6. Mambo muhimu sana ya kuzingatia kuhusu meditation;
1. Meditation siyo zoezi la kidini, japo ilianza na dini ya kibudha, lakini ni kitu ambacho mtu yeyote anaweza kuchagua kufanya.
Na hili nimesahau kwenye faida, meditation inakuwezesha kukua kiroho.
2. Viongozi wote wakubwa na walioweza kuibadili dunia wamekuwa wakifanya meditation
Hata viongozi wa kidini, walianza kwa kumeditate,
Mfano;
Yesu alikuwa akienda milimani kumeditate
Mtume Muhamad alikuwa akienda milimani kumeditate,
Budha alikuwa akienda porini mbali na jamii kumeditate.
Ni kupitia meditation hizi waliweza kupata mapokeo ya kipekee ambayo yaliwawezesha kuwasaidia wengi (enlightment)
3. Kadiri unavyomeditate ndivyo unavyozidi kuona faida zake. Ni zoezi zuri sana kufanya kila siku na mara nyingi kwa siku husika.
4. Ili kuziona faida za meditation, unahitaji kuambatanisha na tabia nyingine nzuri za kiafya, kama kula vyakula vya afya, kufanya mazoezi, kuepuka vilevi.
SEHEMU YA PILI; Bukaza Chachage.
Nilianzeje kumeditate? Mwaka 2002 nilikuwa Sweden, nasoma Lund University. Nilipata shida sana ya msongo wa mawazo kwa sababu hali ya hewa ilikuwa mbaya sana. Nilipofika tu mwezi wa 9 mwishoni jua lilikuwa linazama saa 5 usiku na mimi ninalala jua likizama. Kabla sijazoea hali hiyo majira yakabadilika mwezi wa kumi mwishoni giza kweli kweli na kuna siku huoni jua na mvua au manyunyu kila siku. Na kazi zilikuwa nyingi sana. Nikawa nashindwa kulala kabisa na hali ilikuwa mbaya sana. Ndipo nilikutana na meditation. Nilishauriwa kufanya mazoezi na kule nikafundiswa meditation. Shule ikawa rahisi sana na nikaanza kufanya shughuri zangu nyingine. Kwa kweli toka nianze meditation sikumbuki kushindwA kitu.
Mimi nameditate kila siku kabla ya kulala nusu saa mpaka saa moja na asubuhi nikiamuka kwa saa moja. Kwa hiyo kila siku kuanzia saa 3 usiku nafanya meditation. Na asubuhi ni kuanzia saa 11 – 12. Siku nyingine za weekend naweza hata kumeditate kwa masaa 3-6.
Nikifanya meditation navaa track suit au nguo yoyote ambayo hainibani. Baada ya kula napumzika kidogo kama nusu saa na baada ya hapo naanza kufanya meditation. Huwa ninafanya meditation sehemu hiyo hiyo kila siku.
Nilikuwa nakaa kwenye kiti lakini sasa hivi huwa ninakaa kwenye cusion na nyingine naweka mgongoni na nakunja miguu lotus au nanyosha miguu nisiwe na maumivu yoyote.
Nakaa nimenyoosha mgongo vizuri ni hili ni lazima katika meditation. Navuta pumzi na kuifuatilia na akili yangu huku nikihesabia mpaka 5 napana tumbo na kukaa na pumzi tumboni kwa kuhesabu mpaka 5 na naitoa kwa kuhesabu mpaka 5 na siku nyingine naweza kuhesabu mpaka 10 kuvuta, 10 kukaa nayo na 10 kutoa. Mara moja moja nafanya medi ya kutembea, kula au kuangalia mshumaa.
Ni kweli kabisa tunajua kidogo sana kuhusu potential tuliyonayo. Ukianza kufanya meditation utaanza kuona ukubwa wako. Sisis ni wakubwa kuliko matatizo yote unayoyaona.
Kama alivyosema Kocha wetu Amani imethibitishwa kwa tafiti kabisa bila shaka yoyote kwamba ukifanya meditation kila siku woga unaondoka, kuwa nervous kwa mfano kuongea mbele za watu kunaondoka na msongo wa mawazo (stress) zote huondoka kabisa. Mawazo yote hasi yanaondoka ukifanya mediatation kila siku. Ukifanya meditation na ubinafsi unaondoka.
Kama alivyosema Amani, kikazi meditation inaniongezea umakini na focus kwenye kazi, inaondoa kabisa kuchanganya mambo, inaniongezea sana kumbukumbu, najifunza kwa urahisi sana, kuacha kufanya vitu kwa mazoea (siogopi mabadiliko), nikiwa na mambo mengi ndipo utajua ubora wangu (na utulivu mkubwa sana wa kufanya maamuzi) na zaidi inaniongezea ubunifu. Moja ya vitu ninavyoweza sana na kuzalisha mawazo yoyote yale.
Kwa ujumla unapata utulivu wa kipekee kabisa, unaliwazwa, unapata uvumilivu, unapata uwezo wa ajabu wa kuzuia hasira zako, inaondoa kabisa woga, kila kitu kina kuwa wazi kwako, hata usikivu unaongezeka (Unakuwa sensitive sana), inaongeza kujiamini na kukua na kujitambua uwezo wako
Sasa kama upo tayari kuanza basi fanya yafuatayo:
– Chagua muda wako wa kumeditate huo huo kila siku (Kusudi utengeneze tabia)
-Usinywe vitu kama kahawa kabla ya kumeditate
-Usifanya meditation mara tu baada ya kula. Pumzika kidogo kama nusu saa ndio uanze meditation
-Unaweza kukaa kwenye kiti au kwenye mto wa kochi. Unaweza kukunja miguu au kunyosha usiwe na maumivu kabisa kama alivyoshauri kocha.
-Chagua mahali ambapo ni patulivu kabisa
-Kama vitu vingine inachukua muda kujifunza na kuanza kupata matunda ya meditation, lakini kwa kadri unavyozidi kumeditate ndio muda unapungua na faida zinaanza kuonekana haraka kabisa.
Kwa kumalizia Dalai Lama anasema “If every 8 year old in the world is taught MEDITATION, we will eliminate violence from the world within one generation.”
Virtual mentor wangu kwenye meditation ni Thich Nhat Hanh. Huyu bwana ameandika vitabu vingi sana vya meditation. Katika moja ya mawazo yake anasema ‘MEDITATION can help us embrace our worries, our fear, our anger; and that is very HEALING. We let our own natural capacity of healing do the work.’
Makirita Amani: Kitu cha mwisho kwa leo naomba niwashirikishe app mbili unazoweza kutumia wakati wa meditation, zinakupa muongozo.
Ya kwanza inaitwa HEADSPACE, hii ni burw kudownload na kutumia, ila inakupa siku kumi za kumeditate kwa dakika kumi kila siku, kisha ukitaka zaidi unatakiwa kulipia.
Unaweza kuanza na hii kwa wiki hii ya majaribio. App hii iko poa sana, huwa naitumia.
Ya pili inaitwa STOP, BREATH & THINK, hii ni bure kabisa, nayo pia iko vizuri.
Zote ni rahisi kutumia, na maelekezo yako wazi.
Kuzipata nenda kwenye app store yako kama android nenda plas store, kama iphone nenda kwenye store, search na install app.
KUMBUKUA KUPUMUA.