Hivi Ndivyo Watu Wanavyoua Biashara Au Ajira Zao Wenyewe Na Jinsi Ya Kuepuka.

Kama una biashara na ikafa, au umewahi kuwa na biashara siku za nyuma na ikafa, basi kwa sehemu kubwa sana ni wewe mwenyewe uliua biashara yako. na kama kwa sasa una biashara lakini haifanyi vizuri kama ambavyo ulikuwa unategemea, jua ya kwamba wewe mwenyewe ndiyo sababu kubwa ya biashara yako kukwama.
Pia kwenye ajira, kama umewahi kuajiriwa lakini kazi ile ikaisha, yaani ukafukuzwa au ukaamua wewe mwenyewe kuacha, basi sehemu kubwa ya kilichokufikisha hapo ni wewe mwenyewe. Na kama kwa sasa upo kwenye ajira lakini unaona kama ajira imedumaa, huoni ukikua na wala kipato chako hakikui, kazi imekuchosha na upo tu, basi kuna mambo unayofanya na yanaelekea kumaliza kabisa ajira yako.
Kuna sababu nyingi sana zinazopelekea biashara au ajira kufa. Leo hapa tunakwenda kuangalia sababu moja kubwa sana, ambayo ndiyo imeua biashara na ajira za wengi. Na cha kushangaza sana kuhusu sababu hii ni kwamba inaanza na mtu mwenyewe, na wala haitoki nje ya mtu.
Nyoosha mkono kama umewahi kuona hali kama hii;
Mtu anaanzisha biashara yake, ana malengo na mipango mikubwa, anakuwa na hamasa kubwa sana. Biashara inaanza, anapata wateja wengi, anakazana sana kuwahudumia, na wanafurahia. Lakini baada ya muda wateja wanaanza kulalamika kwamba zile huduma walizokuwa wanapata zamani sasa hivi hawapati tena, na mmoja mmoja wanaanza kuihama biashara. Na hali hii inapotokea mwenye biashara anakazana kuibadili kwa kuzidi kubana mambo kwenye biashara yake.
Au mtu anaajiriwa, mwanzoni anakuwa na hamasa kubwa sana kuhusu ajira yake hiyo. Kwenye usaili aliahidi kwamba atajituma sana kwenye kazi na atafanya kadiri ya uwezo wake kuhakikisha anaongeza thamani. Kazi inaanza na anaweka juhudi kweli, anaongeza thamani. Lakini kadiri muda unavyozidi kwenda mtu anaichoka kazi, anaanza kuona kama juhudi zote anazoweka ni kazi bure, anaanza kuhoji kipato anachopewa na juhudi anazoweka. Kidogo kidogo kazi inapoteza umaarufu kwake, uzalishaji wake unapungua na hatimaye anaacha au kufukuzwa kazi.
Hizi ni hadithi ambazo zipo kwa wengi, zinaweza kuwa na utofauti kwenye mtiririko wa matukio lakini mwanzo na mwisho unafanana kabisa
Je ni kitu gani kinapelekea hali kama hizi?
Matatizo yote haya yanaanzia kwenye eneo moja muhimu sana kwenye biashara au kazi yoyote. Na eneo hili muhimu ni huduma kwa wateja. Watu wengi wanapoingia kwenye biashara na kupata wateja wengi mwanzoni, hujisahau na kufikiri wateja wananunua kwao kwa sababu wapo. Wanasahau kwamba wateja wananunua kwa sababu zao binafsi, kwa sababu wana mahitaji na wamepata wanakoridhishwa nako. Mtu anaposahau au anapokuwa hajui hili muhimu anaanza kuweka mazoea kwenye biashara yake, wateja wanachoka na kutafuta sehemu nyingine ambayo itawatimizia mahitaji yao.
Hata kwenye ajira, wengi wanapoajiriwa mwanzoni wanakuwa wakijua kwamba juhudi zao ndiyo mafanikio ya ajira zao. Na hivyo wanaweka juhudi sana, na wanaona matokeo mazuri. Lakini siku zinapokwenda wanaanza kuzoea kazi na kuona wao ni sehemu ya kazi hiyo. Hivyo wanasahau ule msingi muhimu uliowajenga mwanzo na hivyo kuanza kufanya kwa mazoea. Wanapoanza kufanya kwa mazoea wanapunguza uzalishaji wao na wale wanaotegemea kazi zao wanaanza kuacha kuzitegemea. Hii inamuathiri mwajiriwa mwenyewe na hata mwajiri wake. Inapotokea kwamba kuna mtu mwingine wa kuzalisha vizuri kuliko aliyepo, basi nafasi inakwenda kwake.
Jim Rohn, aliyekuwa mwandishi na mhamasishaji kutoka marekani alikuwa akisisitiza sana hili; unalipwa kulingana na thamani unayopeleka sokoni. Kwa lugha rahisi ni kwamba unalipwa kulingana na thamani unayompatia mteja wako. Iwe ni kwenye biashara au kwenye ajira, kipimo pekee cha malipo yako ni je mteja amenufaikaje na kile ulichofanya? Kwa sababu ni mteja ndiye anayelipa na sehemu ya faida inakuja kwako, iwe ni kwenye biashara yako binafsi au kwenye ajira.
Bila ya mteja hakuna biashara na wala hakuna kazi. Ndiyo maana mteja ni sehemu muhimu sana ya biashara yoyote au kiwanda chochote kinachozalisha, au taasisi yoyote inayotoa huduma zake kwa watu.
Ufanye nini ili kuepuka kuua biashara au ajira yako mwenyewe?
Kama tulivyoona ya kwamba mteja ndiyo nguzo muhimu ya mafanikio kwenye biashara au kazi, basi ni muhimu sana wewe kuwa na maarifa sahihi juu ya utoaji wa huduma bora sana kwa wateja wako. Hili ni eneo ambalo watu wengi huwa hawajifunzi na kuishia kufanya tu kwa mazoea. Mazoea haya yamekuwa yakiathiri sana biashara na hata kazi zao.
Amka Consultants tumekuandalia semina ya UTOAJI WA HUDUMA BORA SANA KWA WATEJA. Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao hivyo unaweza kushiriki popote pale ulipo. Semina itaanza tarehe 02/05/2016 na itaendeshwa kwa siku kumi. Kwenye semina hii utajifunza haya yafuatayo;
1. Kila mtu anauza, je wewe unauza nini?
2. Nani ni mteja wako?
3. Mahitaji ya msingi ya mteja wako.
4. Jinsi ya kutatua hali ya kutoelewana baina yako na mteja wako.
5. Mfanye mteja kuwa rafiki yako.
6. pokea maoni ya wateja wako.
7. Kitu kimoja unachotakiwa kuzingatia sana na kitakunufaisha wewe na mteja wako.
8. Gharama za huduma mbovu kwa wateja wako.
9. Vaa viatu vya mteja wako.
10. Matumizi ya mtandao na teknolojia katika kuboresha huduma kwa wateja.
Karibu sana ushiriki semina hii ambayo itakupa mbinu bora za kutoa huduma bora kwa wateja wako na hivyo kuendelea kufanikiwa kwenye biashara na kazi yako. kushiriki semina hii tuma ada ya ushiriki ambayo ni tsh elfu 20 (20,000/=) kwenye namba zifuatazo; mpesa 0755 953 887, tigo pesa 0717 396 253 namba zote jina ni Amani Makirita. Baada ya kufanya malipo tuma ujumbe kwenye moja ya namba hizo au tuma ujumbe kwa wasap kwenye namba 0717396253. Pia bonyeza maandishi haya na jaza taarifa zako.
Ni wakati sasa wa kuongeza umakini kwenye biashara na kazi yako ili uweze kufikia mafanikio makubwa zaidi. Karibu tujifunze kwa pamoja.
TUPO PAMOJA,
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani.
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: