Kila mmoja wetu kuna kitu ambacho anajulikana kupitia kitu hiko.

Pale watu wanapoongea kitu, wanatumia vitu fulani kutoka kwetu kama mifano.

Tukianzia kwenye eneo lako la kazi, unajulikana kwa nini? Ni kipi ambacho watu wakifanya au kuzungumzia lazima wewe utajwe. Je najulikana kwa kumaliza majukumu yako kwa wakati na kwa viwango vizuri au unajulikana kwa uvivu na kukwepa majukumu? Je unajulikana kama mtu ambaye wengine wakiwa na shida wanaweza kuja kwako na wakapata ushauri mzuri au unajulikana kama mtu ambaye hujali kuhusu wengine?

Tukienda kwenye eneo lako la biashara, ni kipi ambacho watu wanakujua wewe kupitia hiko. Ni namna gani wateja wanaambiana kuhusu biashara yako? je unajulikana kama mfanyabiashara ambaye unatoa thamani na kujali kuhusu wateja? Au unajulikana kama mfanyabiashara anayejali faida tu, mteja akikosea ni juu yake, haikuhusu.

SOMA; FALSAFA MPYA YA MAISHA; TATU MARA TATU, Vitu Vitatu Vyakufanya Kila Siku Ili Kuwa Na Maisha Bora Yenye Furaha Na Mafanikio.

Hata kwenye familia, kuna namna ambavyo wanafamilia wanakuchukulia wewe kama mtoto, baba, mama au ndugu. Je wanakuchukuliaje? Wanakuja kwako kwa lipi?

Hili ni zoezi muhimu la kufanya mara kwa mara kwenye maisha yetu, siyo kwa sababu tunataka watu watuone vizuri, bali tunataka kujua kama tunaiishi ile misingi yetu, ya kuwa na maisha bora kwetu na kwa wanaotuzunguka.

Muhimu ni kwamba tunajulikana kwa matendo yetu, na siyo maneno yetu. Kusema kwamba wewe ni mwaminifu hakukufanyi uwe mwaminifu. Bali pale unapowatendea watu kwa uaminifu, wanasema huyu ni mwaminifu.

Fanya kilicho sahihi wakati wote, na utapata matokeo bora kwako na kwa wanaokuzunguka pia.

TUPO PAMOJA,

KOCHA MAKIRITA AMANI.

www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)