Kitu chochote ambacho tunafanya kwenye maisha yetu, kuna matokeo ya aina mbili; kupata kile tunachotarajia kupata au kupata matokeo tofauti kabisa. Tunaweza kufanikiwa kwenye kile tunachofanya au tunaweza kushindwa.

Haya yote ni matokeo tunayoweza kupata bila ya kujali tunakubaliana nayo au la.

Changamoto yetu kubwa ni kwamba tunapendelea matokeo ya aina moja kuliko aina nyingine. Tunapendelea matokeo yale mazuri kwetu na tunapoyapata tunafurahia. Lakini tunapopata matokeo ya tofauti, tunaona kama ni kisirani kwetu.

Kwa kifupi tumeegemea kwenye matokeo ya aina moja na hii inapelekea sisi kushindwa kujifunza kupitia kila tunachofanya.

Kama tunataka kufanikiwa, kama tunataka kusonga mbele, ni lazima tuwe tayari kuishi na uwezekano wa kupata matokeo yoyote kati ya hayo mawili. Ni lazima tuwe tayari kupokea matokeo tunayopata na kujifunza zaidi kupitia matokeo hayo, iwe ni mazuri au mabaya.

SOMA; BIASHARA LEO; Kwa Mabadiliko Yanayoendelea Nchini, Ni Lazima Tubadili Mbinu Zetu Za Kibiashara Kama Tunataka Kufanikiwa.

Unapokuwa na aina hii ya fikra, utaona kila hatua ya maisha yako kama sehemu ya kujifunza na kujiandaa kupokea makubwa ya baadaye.

Tarajia matokeo mazuri, ila pia kuwa tayari kupokea matokeo mabaya. Ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku.

TUPO PAMOJA,

KOCHA MAKIRITA AMANI.

www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)