Kama unataka kuwa bora zaidi ya ulivyo sasa, kuna uwekezaji mmoja muhimu sana ambao huwezi kukwepa kuufanya. Uwekezaji huu ni kuwekeza kwako wewe binafsi, kuongeza maarifa, ujuzi na hatimaye uzoefu wako.
Kama hakuna maarifa mapya unayopata, utaendelea kufanya unavyofanya sasa na hivyo kuendelea kupata unachopata sasa. Ili kupata matokeo ya tofauti na unayopata sasa, unahitaji kufanya uwekezaji mkubwa kwako binafsi.
Uwekezaji wowote unahitaji kuwa na rasilimali, na kwenye uwekezaji wako wewe binafsi, unahitaji kuwa na rasilimali mbili muhimu sana ambazo tunakwenda kuzijadili hapa.
Rasilimali ya kwanza ni fedha.
Ili upate maarifa mapya na bora, ili upate ujuzi ambao utakuwezesha kuwa bora zaidi ya ulivyo sasa, unahitaji kuwa na fedha. Uzuri wa zama hizi ni kwamba huhitaji kuwa na fedha nyingi sana, kwa sababu hata kama una kiasi kidogo, bado unaweza kupata maarifa na ujuzi mwingi unaotaka.
Kupata maarifa na ujuzi, unahitaji kununua vitabu (vingi), unahitaji kuhudhuria semina na makongamano, unahitaji kujiandikisha kwenye kozi mbalimbali na pia inapobidi, unahitaji kurudi darasani ukasome.
Rasilimali ya pili ni muda.
Unahitaji muda w akupata maarifa na ujuzi unaotaka, kama ni vitabu unahitaji kutenga muda wa kuvisoma, kama ni semina au mafunzo, unahitaji kutenga muda kuhudhuria. Haijalishi unaweza kulipa kiasi gani, kama huwezi kutenga muda wa kuyapata maarifa hayo, hakuna unachoweza kubadilisha.
Unahitaji kutenga muda kila siku wa kujifunza na kujiendeleza kwenye kile unachofanya. Pia unahitaji kutenga muda wa kuhudhuria semina mbalimbali ambazo zinahusiana na kile unachofanya.
Ufanye nini?
Tenga bajeti nzuri ya fedha na muda wako kila mwaka kwa ajili ya kujifunza na kujiendeleza. Kila siku soma angalau kwa nusu saa kitu kinachokuongezea maarifa au hamasa kwenye kile unachofanya.
Uanzie wapi?
Kujifunza kila siku bonyeza hapa, kuhudhuria semina bonyeza hapa.
TUPO PAMOJA,
KOCHA MAKIRITA AMANI.
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)