Unaweza usielewe lakini unatakiwa kufurahia vikwazo unavyokutana navyo kwenye safari yako ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa. Iwe ni kwenye kazi, biashara na hata maisha kwa ujumla.

Kwa nini?

Kwa sababu vikwazo hivyo ndiyo vinawazuia wengi kufanikiwa. Vikwazo hivyo ndiyo vinawafanya wengi kukata tamaa na kushindwa kuchukua hatua. Vikwazo hivi ndiyo vinawafanya wachache pekee wafanikiwe, na hivyo ushindani kuwa mdogo kwenye mafanikio hayo.

Unapofanya kitu ambacho hakina vikwazo, unakuwa kwenye ushindani mkali sana, kwa sababu kila mtu anakuwa anafanya kitu hicho.

Matatizo ni vikwazo ndiyo mlango mkuu wa mafanikio. Mlango huu unapima nani amejitoa kweli na yupo tayari kuufungua, pia unawaweka nje wale ambao hawajajitoa na kuwa tayari kuufungua ili wafanikiwe.

SOMA;  FALSAFA MPYA YA MAISHA; Changamoto Za Kuondoka Kwenye Vifungo Vya Maisha Na Kupata Uhuru Wa Maisha.

Unapoona sehemu ina changamoto, ing’ang’anie, kwani ukiweza kuvuka changamoto hizo, utafika mbali sana.

Unapokutana na vikwazo, usikimbie, badala yake vikabili na vitakuwezesha kukua ziadi.

TUPO PAMOJA,

KOCHA MAKIRITA AMANI.

www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)