Je unaweza kula chakula kizuri ambacho ndani yake kuna mchanga?
Je ukiambiwa uchague dhahabu ambayo ni safi kwa asilimia 100 na dhahabu ambayo ni safi kwa asilimia 50, utachagua dhahabu ipi?
Linapokuja swala la chakula au urembo, tunahakikisha tunapata kilicho safi kabisa. Usafi ni kipaumbele chetu cha kwanza kuhakikisha tunapata kile ambacho ni bora kabisa.

Sasa tuje kwenye kitu kimoja muhimu sana katika maisha yetu, kitu ambacho kinaongoza maisha yetu. Kitu hiki ni akili na mawazo yetu. Huu ndiyo msingi mkuu wa maisha yetu.
Swali ni je tunazingatia usafi wake kama tunavyozingatia kwenye chakula na urembo? Je tunahakikisha akili na mawazo yetu yanakuwa safi kwa asilimia 100?
Ni muhimu kujiuliza hivi kwa sababu watu wengi wamekuwa wanajisahau na kuruhusu akili na mawazo yao kuchafuliwa na yeyote anayeamua kufanya hivyo. Wanaruhusu watu kuja na uchafu wao na kuumwaga kwenye akili na mawazo yao. Kwa njia hii wanashindwa kufikiri yale ambayo ni muhimu sana kwao na kushindwa kufanikiwa.
Uchafu wa akili ni nini?
1. Mawazo yoyote hasi.
2. Habari zozote hasi.
3. Ulevi wa aina yoyote ile.
4. Uteja wa aina yoyote ile.
5. Kufuatilia mambo ambayo hayana umuhimu wowote kwako.
Epuka kuchafua akili yako, weka juhudi kuhakikisha akili yako inakuwa safi muda wote, usafi wa asilimia 100. Fanya hivi kwa kuepuka uchafu wa akili na pia kuisafisha kwa kujifunza na kujihamasisha, pia kwa kuweka malengo na mipango na kuifanyia kazi kila siku.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK