Acha Kusimama…Fanya Kitu Cha Kubadili Maisha Yako.

Kila kitu hakitakuwa kibaya katika maisha yako, wala maisha yako ya mafanikio hayatafika mwisho, eti kwa sababu kwa sasa unapitia katika hali ngumu sana ya kimaisha.
Changamoto unazozipitia katika maisha, zisikufanye ikafika mahali ukajiona wewe hufai, changomoto hizo zisikufanye pia ukajiona umechanganyikiwa na huwezi tena, nafasi ya kubadilisha maisha yako ipo pale pale.
Ni rahisi kujiona husogei katika maisha yako kwa sababu ya hali unayoyapitia. Unachotakiwa kufanya hutakiwi kulidhika na hali hiyo ulipo na kujihalalishia kwamba mimi basi, kipo kitu cha kufanya.
Siku zote wanasema hatua hutengeneza mwendo, pamoja na hali mbaya unayopitia, pamoja na magumu unayopitia, ila fanya kitu kwa kuanza kupanga mipango upya ya nini tena ufanye ili kuweza kufanikiwa.

Hakikisha unabadili maisha yako.
Acha kuendelea kufanya kosa juu ya kosa, acha kusimama kwa namna yoyote ile, kama mambo yako unaona hayaendi sawa, fanya kitu cha kubadili maisha yako mara moja.
Maisha yako kumbuka hayawezi kubaki hivyo hata iweje, ipo nafasi ya kujaribu tena. Nafasi hiyo hana mtu mwingine zaidi yako wewe, ambaye unatakiwa kuitumia na kuisimamia hadi kuona unafanikiwa.
Kutokufanya kitu chochote wakati maisha yako unaona yanakwenda hovyo, haitakusidia kitu. Acha kuniambia kwamba umejaribu sana umeshindwa, acha kuniambia umefanya sana bila matokeo, fanya kitu cha kubadili maisha yako sasa.
Kufanya kitu cha kubadili maisha yako na kujifunza kutokusimama, ni jambo ambalo unatakiwa kulifanyia kazi kila siku bila kuchoka. Hali yoyote unayokumbana nayo isikutishe amua kuibadili.
Unapoona watu waliofanikiwa, hawakupata mafanikio yao hivi hivi tu, bali mafaniko yao waliyapata kwa kwa kuendelea kufanya kitu katika maisha yao na wala sio kusimama kusikilizia maumivu ya kushindwa.
Ikiwa utakuwa mtumwa na kusimama…na kusikilizia maumivu fulani ya kushindwa na kuacha kufanya kitu  cha kubadili hali uliyonayo kwenye maisha yako…nakupa uhakika utajikwamisha mwenyewe na utaenda kufanya maisha yako yawe mabovu.
Washindi wote katika mafanikio wanakuja kwa kutenda…fanya kitu katika maisha yako, hata kama kitu hicho ni kidogo, wewe fanya. Wahenga walisema kidogo kidogo hujaza kibaba, kwa kufanya hivyo hivyo utaleta mabadiliko ya maisha yako.  
Kumbuka hili siku zote na liweke katika hatua ya utendaji, utabadilisha maisha yako sana na kuwa ya mafanikio makubwa.
Tunakutakia siku njema na kila la kheri.
Endelea kuchota maarifa ya kuboresha maisha yako kwa kutembelea AMKA MTANZANIA na DIRAYA MAFANIKIO kila siku, kwani hizi ndizo nyumba halisi za mfanikio yako ya kudumu.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: