Habari za asubuhi ya leo rafiki yangu?
Hongera kwa nafasi hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora kwetu kwenda kuweka juhudi zaidi ili tuweze kupata matokeo bora zaidi. Tutumie siku hiibya leo vizuri.
Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu PARADOX,
Paradox ni ile hali ambayo kitu kinatokea tofauti ha tunavyotegemea. Yaani ni kama vitu vinakuwa kinyume na matarajio au matagemeo yetu.
Kwa mfano, utakuta watu wenye afya bora ndiyo wanazingatia kanuni za afya kuliko wale ambao wana afya mbovu, ambao ndiyo wangepaswa kuzingatia kanuni za afya zaidi.
Au ikija kwenye swala la fedha, unakuta matajiri ndiyo wanaokazana zaidi kuzipata fedha kuliko hata masikini, ambao ndiyo walipaswa kuweka juhudi zaidi ili kutoka pale alipo.
Pia utakuwa wale wenye busara wakipenda kujifunza zaidi, na kujua hawajui, lakini wapumbavu hawataki kabisa kujifunza na wakiamini wanajua kila kitu.
Ukiangalia upande wa muda, wale ambao hawana muda kabisa, ndiyo ambao wanatekeleza mengi na makubwa. Ila wale wenye muda mwingi na wa kutosha, hakuna hata kikubwa wanachoweza kufanya.
Kuna paradox nyingi zinazotokea kwenye maisha yetu ya kila siku, ila nyingi zinatufanya tuahindwe kufikia mafanikio.
Hivyo asubuhi ya leo tafakari hili kwa kina, jiangalie ni mambo gani ambayo ndiyo unapaswa kuyazingatia aana ila kwa sasa huyazingatii?
Hayo ndiyo yanakuzuia wewe kufanikiwa.
Fanya kile unachopaswa kufanya, weka juhudi zaidi bila ya kujali umefika wapi. Jifunze zaidi kila siku, usifike mahali na kuona umeshajua kila kitu.
Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
http://www.makirita.info