Hatua Muhimu Inayorukwa Na Watu Wengi Katika Mahusiano Ya Uchumba Na Ndoa.

Habari ya wakati huu mpendwa rafiki na msomaji wa Amka Mtanzania? Ni matumaini yangu hujambo na unaendelea vizuri kuwajibika kuhakikisha ya kwamba unapata kile unachokihitaji kwenye maisha yako. Hongera sana rafiki kwa kuendelea kuwa pamoja nami katika safu hii ya kujifunza mambo mbalimbali yanayotusaidia kupata maarifa na kuboresha maisha yetu kwa ujumla. Rafiki kujitegemea siyo kujitosheleza bado unahitaji watu mbalimbali ili uweze kusonga mbele zaidi. Napenda kutumia nafasi hii kukualika mpenzi msomaji wa mtandao wa amka Mtanzania katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza kwa pamoja.

 

Katika makala yetu ya leo tutajifunza hatua muhimu inayorukwa na watu wengi katika mahusiano ya uchumba na ndoa. Karibu rafiki tujifunze kwa pamoja somo zuri nililokuandalia siku hii ya leo. 

Kabla ya kuingia katika mahusiano ya uchumba na ndoa kuna hatua muhimu sana inayorukwa na watu wengi. Unakuta watu wengi wanaanza hatua ya pili ya uchumba bila kupitia hatua hiyo ndio maana matatizo mengi huibuka pindi watu wanapokuwa wanaingia katika maisha ya ndoa. Hatua muhimu inayorukwa na watu wengi ni urafiki. Kabla ya kuingia katika mahusiano ya uchumba na ndoa ni muhimu kupitia hatua hii ya msingi katika mahusiano yako. Urafiki ndio msingi wa uchumba wenu na ndoa yenu hivyo kuna faida nyingi za kuanza na hatua ya urafiki kabla ya kuingia kwenye mahusiano ya uchumba na ndoa.

SOMA;  Vikwazo Vitano(5) Vinavyoharibu Mahusiano Yetu Na Ndoa Zetu Na Jinsi Ya Kuviepuka.

Faida ya kwanza ni kuchunguzana. Katika hatua hii muhimu ukiwa na rafiki wako wa kike au wa kiume hii ndio sehemu nzuri ya kuchunguzana kuliko ukiwa katika mahusiano ya uchumba au ndoa. Kwanini ? kwa sababu hatua hii ya urafiki mnakuwa huru kuchunguzana kuliko ukiwa katika mahusiano ya uchumba kwani watu wengi kwenye mahusiano ya uchumba huwa wanavaa uso wa bandia ili kuficha makucha yake ili aonekane vizuri kwa mwenzake. Lakini kama una malengo na mtu Fulani anza naye katika hatua ya urafiki wa kawaida na wala usimwambie shabaha yako ni nini bali hii inakuwa ni siri yako wewe mwenyewe tu.

Mchunguze taratibu katika mahusiano yenu ya kirafiki pata muda wa kutosha wa kujiridhisha na mwenendo wake mzima wa maisha. Chunguza tamaduni zao, jifunze, mwangalie kama ni mtu wa namna gani ni mvivu au mchapakazi yaani chunguza kila kitu baada ya kujiridhisha na kuona yuko vizuri na anakufaa sasa unaweza kumwambia kuwa unamhitaji na ndio mnaanza mahusiano ya uchumba. Watu wanaoanza mahusiano bila kupitia hatua ya urafiki wa kawaida huwa inawasumbua mbeleni kwani inakuwa inachukua muda kila mmoja kuonesha udhaifu wake. Kila mtu anajitahidi kuficha udhaifu aonekane vizuri mbele ya mwenzake.

SOMA; Hawa Ndio Maadui Wakubwa Wawili Wa Uchumba Au Ndoa Yako.

Faida ya pili, itakusaidia kufanya maamuzi sahihi. Baada ya kumchunguza rafiki yako awe ni wa kike au wakiume na ukagundua rafiki yako yuko vizuri umeridhishwa na mwenendo wake wa tabia sasa ukaona ni vema umwambie ukweli kuwa una mwitaji katika mahusiano ya uchumba. 

Hapa utapata faida sana kufanya maamuzi sahihi kwa kuwa ulikuwa umeshafanya uchunguzi mzuri juu ya rafiki yako pindi mko katika urafiki wa kawaida ambapo yeye alikuwa hajui lengo lako wewe la kuwa na urafiki na yeye ni kumchunguza kwanza ili muingie katika mahusiano ya uchumba na hatimaye ndoa.

Kama unataka umpate mwenza mzuri katika maisha yako ni vema mkaanzia katika hatua hii muhimu ya urafiki bila kumuonesha wazi kuwa unamhitaji na utakuja kumwambia pale lengo lako la uchunguzi limekamilika. Kwa njia hii ni ngumu sana kuficha tabia zake kwani utakua na uhuru mkubwa wa kuchunguzana kuliko kuruka hatua ya urafiki na kukimbilia uchumba na hatimaye ndoa.

SOMA; Tabia Nane (8) Zinazo Dhoofisha Mahusiano Yako Ya Ndoa, Uchumba Na Mengine Na Hatua Za Kuchukua.

Hatua ya kuchukua; kama unataka kuingia katika mahusiano ya uchumba na ndoa tafadhali fuata hatua hizi tatu. Ya kwanza ni urafiki, ya pili ni uchumba na ya mwisho ndio ndoa yenyewe. 

Angalizo ni kwamba unapokuwa katika mahusiano ya urafiki usimwambie mwenzako kuwa una mwitaji katika mahusiano mengine bali wewe tumia kama njia ya kuchunguza kwanza na baada ya kuona yuko vizuri ndio unamwimbia sasa. Njia hii itakusaidia sana rafiki yangu ambaye unataka kuingia katika mahusiano ya uchumba na ndoa.

Kwa kuhitimisha, huwezi kumpata mtu sahihi katika maisha ya mahusiano yoyote yale kama wewe siyo mtu sahihi. Hapa kanuni ya dhahabu inahusika, kanuni ya asili inahusika hivyo usitegemee kupokea kama hatuoi na kaa ukijua ya kwamba unavuna kile ulichopanda kamwe huwezi kupata matokeo tofauti. Maisha ni kupanga na kuchagua na mwenye maamuzi ya mwisho juu ya mahusiano yako ni wewe mwenyewe.

Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com, kessydeo@mtaalamu.net au unaweza kutembelea tovuti yake, www.mtaalamu.net/kessydeo ,www.actualizeyourdream.blogspot.com

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: