Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi zaidi ili kupata matokeo bora zaidi.
Tutumie nafasi ya leo vizuri rafiki.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu HADITHI YA MAISHA YAKO,
Kila mtu ana hadithi fulani ya maisha yake,
Kila mtu kuna namna anavyojiona kwenye maisha yake.
Kuna vitu ambavyo anajua anaweza kufanya na vingine hawezi kufanya.
Hadithi hii ya maisha yako ambayo unayo,nina nguvu kubwa sana kwenye kuyaongoza maisha yako.
Kwa kifupi, maisha yako hayawezi kuwa bora zaidi ya hadithi ya maisha yako ambayo unayo.
Juhudi zote unazoweka, zitaishia kukuletea matokeo yanayoendana na ile hadithi ya maisha yako.
Hivyo kabla haya ya kuweka juhudi kubwa kwenye maisha yako, hebu anza badili hadithi ya maisha yako. Hebu kwanza tangeneza hadithi mpya ya maisha mapya unayotaka. Na kila siku jiambie hadithi hii mpya. Kila siku jione kwenye nafasi hii mpya.
Kwa hadithi mpya, unaweza kutengeneza maisha mapya.
Nakutakia siku njema sana rafiki.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
http://www.makirita.info