Hatua Muhimu Za Kufuata Ili Kutengeneza Kipato Kikubwa.

Katika nyakati za sasa, wakati ambapo dunia inakwenda kwa kasi na hali ya uchumi ikubadilika sana, ipo haja ya kila mtu kuweza kujifunza namna ya kuweza kutengeneza kipato kikubwa na cha kudumu.
Hiyo iko hivyo kwa sababu, bila kufanya hivyo, utaachwa nyuma sana kimafanikio na utajikuta ukiwa ni mtu wa pale pale, miaka na miaka. Una anzaje kujitengenezea kipato kikubwa wakati pengine mtaji wako ni mdogo?
Zifuatazo ni hatua muhimu za kufuata ili kutengeneza kipato kikubwa.
  1. Anza na kidogo.
Katika harakati za kutengeneza kipato cha kikubwa na cha kudumu ni vyema ukajifunza kuanza na kidogo. Anzia pale ulipo ili kutafuta mafanikio yako. Chochote ambacho unaona kinakufaa kifanya, hata bila kuona haya.
Watu waliofanikiwa si kwamba walianza na mambo makubwa sana, hapana. Mara nyingi ni watu waliomua kukubali kukaa chini na kuanza na kidogo kile walichonacho ili kufikia  mafanikio yao.

Ni jukumu hilo hilo ambalo unaweza hata wewe ukalichukua na kuanza na kidogo ulichonacho. Acha kusubiri sana mpaka kila kitu kikamilike ndio uanze kufanya. Ukifanya hivyo, yaani kuendelea kusubiri utakuwa unajichelewesha mwenyewe kufanikiwa.
2. Jenga fikra chanya.
Hautaweza kutengeneza kipato kikubwa na  kufanikiwa kama kila wakati fikra zako zipo hasi, hasa linapokuja suala linalohusiana na mambo ya fedha. Ni lazima fikra zako ziwe chanya na kuamini kwamba una uwezo wa kutengeneza  pesa.
Acha kuendelea kung’ang’ania fikra mgando ambazo hata hazikusadii kitu, zaidi zinakukwamisha sana kufanikiwa. Watu waliofanikiwa kipesa na kutengeneza pesa nyingi, kila wakati huamini sana wao ni watu wa pesa.
Kwa kuamni kila siku na kuendelea kufanyia kazi yale wanayoyafanya bila kuchoka hujikuta wakiwa na pesa nyingi sana katika maisha yao. Kama leo hii unataka kutengeneza kipato kikubwa, jenga fikra chanya juu ya pesa na utafanikiwa.
3. Weka mipango imara.
Silaha pekee ya kuweza kufanikisha kujenga kipato kikubwa na cha uhakika ni kwa wewe kuhakikisha unakuwa na mipango ya kutengeneza kipato hicho. Ni muhimu sana kujiwekea mipango imara ili ikusaidie kutimiza lengo lako.
Kwa mfano, unaweza ukaweka mipango ya kuwekeza vitega uchumi vya aina tofauti tofauti ambavyo vitakusaidia katika kutengeneza kipato kikubwa. Ukishaweka mipango hiyo unaiweka kwenye utekelezaji.
Watu wenye mafanikio makubwa ndvyo ambavyo hujiwekea mipango yao kwa staili hiyo karibu kila siku. Lakini hawaishii kuweka mipango hiyo bali huchukua jukumu la kuifatilia kial siku. Hicho ndicho kitu unachotakiwa kukifanya ili ufanikiwe pia.
4. Kuwa mvumilivu.
Kila mafanikio yanahitaji uvumulivu wa aina fulani ili uweze kuyapata. Hakuna mafaniko ambayo unaweza eti ukayapata bila kuvumilia. Kipo kipindi ambacho kwa vyovyote vile ni lazima usibiri.
Hivyo wakati umejiwekea mipango na mikakati yako ya kukuwezesha kufanikiwa, tambua unatakiwa kuwa mpole kwa kukaa chini na kusubiri mchakato wa mafanikio yako kuwezekana.
Kila mtu aliye na mafanikio leo hii ukimuuliza ni lazima atakwamba alivumilia kwa namna fulani hivi na hakuyapata mafanikio hayo mara moja. Ili nawe uweze kujenga kipato kikubwa unahitaji uvumilivu wa kutosha. Jipe muda wa kuvumilia.
Kitu unachotakiwa ukijue mapema ili uweze kutengeneza kipato kikubwa ni kwamba, kipato hicho huwa hakitengenezwi kwa bahati mbaya. Mara nyingi huwa ipo misingi au hatua unazotakiwa  uzifuate kama ambavyo tulivyojadili kujadili.
Kumbuka zaidi ili uweze kutengeneza kipato kikubwa, unahitaji kuanza na kidogo, kujenga fikra chanya juu ya pesa, kuweka mipango imara na wewe kuwa mvumilivu. Ukiweza kuzingata mambo hayo. Hilo halina shaka, tayari utakuwa na uhakika wa kutengeneza kipato kikubwa.
Endelea kutembelea www.amkamtanzania.com kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s