Hongera kwa siku nyingine nzuri sana ya leo rafiki.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa zaidi ili kupata matokeo bora zaidi.
Tumia muda wa leo vizuri kwa sababu ukishapita hautorudi tena.

img_20161112_091656

Asubuhi ya leo tutafakari ni mtu gani ambaye unamwangalia.
Japokuwa unahitaji kuishi maisha yako, na kupanga mafanikio kwako yana maana gani, bado unahitaji kuwa na mtu ambaye unamwangalia.
Huyu ni mtu ambaye anakuhamasisha na kukuvutia wewe uwe kama yeye.
Ni mtu ambaye ameweka viwango ambavyo na wewe ungependa kuviishi.

Watu wa aina hii ni muhimu sana kwetu, japo hatuhitaji maisha yetu yaende kama yao, lakini tunataka tuweze kufikia viwango ambavyo nao wamefikia
Je hapo ulipo una mtu wa aina hii?
Kama yupo vizuri sana, kama hayupo kuna kitu unapoteza, kaa chini na chagua ni mtu gani unaweza kuwa unamwangalia.
Anaweza kuwa mtu wa karibu au hata wa mbali,
Anaweza kuwa hai au hata amekufa.
Muhimu ni ujue viwango vikubwa alivyojiwekea kwenye maisha yake na kuviishi.
Mafanikio ya watu hawa ni chachu kubwa sana kwetu, hamasa ya kutufanya tuweke juhudi zaidi.

Nakutakia siku njema sana ya leo.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
http://www.makirita.info