Habari za asubuhi ya leo rafiki yangu?
Hongera kwa siku hii nzuri sana ya leo,
Siku bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo makubwa. Tutumie siku hii ya leo vizuri ili tuweze kupata matokeo bora kabisa.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu yale mambo ambayo tunayafanya.
Huwa sielewi pale ninapokutana na mtu anafanya kitu kwa uhovyo kabisa kwa sababu tu hapendi kufanya kitu hicho, au analipwa kidogo kulinganisha na anachofanya.
Huwa sielewi kwa sababu naona jinsi ambavyo mtu anapoteza muda wake na maisha yake kwa kitu ambachonyeye mwenyewe hakijali, na hakuna mwingine yeyote anayekijali.
Asubuhi hii ya leo nataka nikuambie ya kwamba, KAMA UMECHAGUA AU KUAMUA KUFANYA KITU, BASI KIFANYE VIZURI MNO. WEKA KILA ULICHONACHO KWENYE KILE ULICHOCHAGUA KUFANYA.
Fanya vizuri siyo tu kwa sababu ya wale unaowafanyia, bali kwa sababi zako binafsi. Unapofanya kitu kizuri kwa wengine, ambacho kinawasaidia, unakuwa muhimu kwao na unajiamini kutokana na mchango unaotoa kwa wengine.
Lakini unapofanya kitu kwa uhovyo, hakuna anayekijali ma hata wewe mwenyewe hutokijali wala hutojijali. Hutaona umuhimu wako kwa wengine na hii inapelekea wewe kukata tamaa na kuona mambo hayawezekani.
Chochote ambacho umeruhusu mikono yako ikishike, kifanye kwa ubora wa hali ya juu sana. Usiangalie unalipwa kiasi gani, usiangalie nani anakuona, bali unachohitaji kuangalia ni mchango unaoutoa kwa wengine kupitia unachofanya. Angalia thamani kubwa unayotoa kwa wengine. Ukishajali kuhusu thamani, mengine yote yatakwenda vizuri sana.
Rafiki yangu, leo nenda kwenye kazi au biashara yako ukiwa na mtazamo tofauti wa ufanyaji. Leo dhamiria kuweka thamani kubwa kw akila unachofanya. Hakikisha kila anayekutana na wewe leo, anaondoka akiwa bora zaidi ya alivyokuwa kabla ya kukutana na wewe.
Fanya hivi na uone kama maishs yako yatabaki hapo yalipo.
Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki yako
#KochaMakirita