Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo rafiki.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora.

img-20161217-wa0002
Kumbuka msingi wetu muhimu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA.
Kika unachofanya siku ya leo, usiache msingi huo muhimu nyuma.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu MWANZO MGUMU.
Mwanzo wa kila kitu unachoanza kufanya huwa ni mgumu,
Ni mgumu kwa sababu hujazoea
Pia ni mgumu kwa sababu kuna vitu vingi hujui.
Halafu unakuwa mgumu zaidi pale unapokutana na changamoto, ambazo huwa hazikwepeki.

Ugumu wa mwanzo umewazuia wengi kuanza,
Ugumu wa mwanzo umewakatisha wengi waliokuwa wameanza.
Na ugumu wa mwanzo umewatenganisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa.

Leo nakupa dawa ya ugumu wa mwanzo rafiki yangu,
Na dawa hii ni kuanza kufanya,
Wewe anza kufanya, na usianze tu, endelea kufanya.
Kubali kuanza kidogo, anzia chini kabisa na kila siku piga hatua ya ziada kuliko ulivyopiga jana.
Kila kinachoanza kinahitaji nguvu kubwa kuliko kuendelea, hata mashine na magari,
Hivyo kuwa na nguvu hii ya kuanza na endelea kufanya, usikubali kurudi nyuma.
Chochote unachotaka kufanya, popote unapotaka kufika, anza kufanya, anza safari.
Kama wanafalsafa wanavyosema, SAFARI YA MAILI ELFU MOJA INAANZA NA HATUA MOJA.
Au kama NIKE wanavyosema, JUST DO IT.
Usiendelee kusubiri, hakuna kitakachokuwa rahisi, ANZA SASA.

Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.