Uongo Mkubwa Unaojidanganya Kila Siku Na Unakupotezea Mafanikio Yako Kabisa.

Katika hali ya kawaida kwenye maisha unaweza ukawa unajidanganya sana kwenye baadhi ya mambo kwa muda mrefu nakufanya ukashindwa kufanikiwa hata bila wewe mwenyewe kujua kwa nini unashindwa.
Hili mara nyingi linatokea kwa mtu pengine unakuwa hujui, hivyo hujikuta umebeba uongo mwingi sana kwenye maisha yako ambao unakurudisha nyuma kila siku.  Kwa kila hatua unazo jaribu kupiga unashangaa haziendi ila kwa sababu ya uongo huo.
Kwa kuwa lengo letu kama amkamtanzania ni kutaka kuona wewe rafiki yetu unafanikiwa, leo katika siku ya leo tunaomba tujifunze pamoja uongo mkubwa ambao umekuwa ukipoteza mafanikio yako kabisa.
Bila kupoteza muda fuatana nasi katika makala haya kuweza kujua aina hii ya uongo, yaani kama utakuwa nao sana, basi ujue moja kwa moja utakuwa upo kwenye hali mbaya ya kukosa mafanikio yako.
1. ‘Nina  muda mwingi wa kutosha.’
Wengi wanajidanganya na kuacha kufanya majukumu ambayo walitakiwa kuyafanya sasa kwa kujiona kwamba wana muda wa kutosha. Kwa msingi huo, huona mambo hayo hata  kwa wakati mwingine wanaweza kuyafanya pia.
Utakuta kwa mfano mtu allikuwa ana jambo ambalo alitakiwa kulifanya sasa, lakini atakwambia ngoja nitalifanya kesho, ukimuuliza kwa nini atakwambuia muda bado ninao nitafanya tu.
Kama unaendelea kujidanganya hivi kwa kuona kwamba bado muda unao wa kuweza kukusaidia kufanikiwa utapotea. Muda wako ulionao ni kidogo sana. Kila dakika unayoipata itumie rafiki ili ikupe mafanikio.
Kila siku ukiendelea kujificha  chini ya mwavuli wa kusema muda ninao utakuja kushtuka umri umekwenda na hakuna kikubwa  ulichokifanya. Hivyo kwa vyovyote vile acha kujidanya muda unao mwingi. Chukua hatua mara moja.
2. ‘Nitafanya nikijisikia.’
Kuna wakatti katika safari mafanikio ni rahisi sana kujikuta ama kujiona mambo sasa yanakuwa kama hayaendi, au hujisikii kabisa kufanya kitu chochote . Hali kama hii hutokea sana tena sana kwa wengi.
Unapotokewa na hali kama hii ni rahisi kuweza kujidanganya na kusema nitafanya nikijisikia kufanya. Ukiona unasema hivyo naomba nikwambie unaweza ukawa upo kwenye hatari kubwa sana pengine ya kutokufanya kabisa.
Mafanikio yoyote yale hayaji kwa kufanya kwa kujisikia. Hata uwe katika wakati mgumu vipi, kama kuna kitu unatakiwa kukifanya hebu kuifanye kitu hicho. Hamasa ya kukifanya hata kama haipo itakuja wakati unaeendelea kufanya.
Kwa namna yoyote ile acha kujidanganya na kusema nitafanya nikijisikia. Ukifanya hivyo basi uelewe pia utakuwa unajiwekea uongo ambao mwisho wa siku utakupotezea mafanikio yako kwa ujumla.
 3. ‘Ni hatari sana kufanya jambo jipya.’
Pia umekuwa ukidangana kwa kuona ni hatari sana kwa kuanza kufanya jambo jipya, ndio maana wasiwasi mwingi umekuwa ukikujaa. Kila hatua ukitaka kuchukua unaogopa sana.
Hivyo haitoshi hata pale unapataka kuchukua hatua za kujitoa mhanga ama kuchukua ‘risk’ umekuwa ukiona kama vile ni mtu ambaye unakwenda kupoteza moja kwa moja kwa kufanya kitu hicho ambacho hujawahi kukifanya.
Huu pia  ni uongo mwingine ambao umekufanya ushindwe kuchukua hatua za mafanikio yako kwa makusudi. Hakuna hatari yoyote ambaye unaweza ukasema ni kubwa sana katika kufanya jambo jipya kiasi kwamba uogope hivyo.
Hivyo, huna haja ya kuendelea kubeba hofu ambazo zisizo na msingi na ukajikuta unaacha fursa muhimu ambazo zingeweza kukusaidia kupiga hatua katika maisha yako kimafanikio.
4. ‘Watu wenye mafanikio wameridhika.’
Mbali nakujiona kwamba una muda mwingi wa kutosha pia unaendelea kujidanganya kwa kuona kwamba watu wenye mafanikio wameridhika na unaona kama hawatumii nguvvu nyingine kufanikiwa.
Kwa kuona hivyo, nawe kwa mafanikio madogo unayoyapata yanakulewesha na kuanza kujiona wewe tena ndiyo basi umefika, hivyo unataka na wewe ujibebeshe mzigo wa kuridhika wakati kumbee safari bado.
Kitu usichokijua  na ambacho naweza kusema kipo nyuma ya pazia la watu wenye mafanikio, ni kwamba wanaweka juhudi sana kila siku, usiku na mchana kuhakikisha mpaka wanafanikiwa. Hawajakaa na kijiachia kama unavyofikiri.
Kwa kuhitimisha makala haya, huo ndio uongo mkubwa ambao unajidangany sana kwenye maisha na unakupelekea ushindwe kupiga hatua sahihi za kimafanikio. Epuka uongo huo na anza kujenga mafanikio yako leo kwa uhakika.
Endelea kujifunza kupitia www.amkamtanzania.com kila siku.
Kwa makala nyingine nzuri za mafanikio na maishja pia tembelea dirayamafanikio.blogspot.comkubadili fikira na mwelekeo wa maisha yako.
Tunakutakia kila la kheri,
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,

One thought on “Uongo Mkubwa Unaojidanganya Kila Siku Na Unakupotezea Mafanikio Yako Kabisa.

Add yours

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: