Hongera rafiki kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi nzuri kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora kabisa.

img-20161217-wa0002
Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana siku ya leo na nyingi zijazo.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu KULIKO JANA…
Chochote unachofanya leo, hakikisha unakifanya kwa ubora zaidi kuliko jana.
Unavyoishi leo, ishi vizuri zaidi kuliko jana.
Imalize siku ya leo ukiwa umejifunza zaidi kuliko jana.
Leo weka juhudi zaidi kuliko jana.

Maisha yanasonga mbele, hayarudi nyuma.
Hivyo kama jana ilikuwa bora zaidi kwako kuliko leo, basi wewe umeanza kurudi nyuma.
Kama leo ni afadhali ya jana kwako, basi umeacha kukua na umeanza kupotea.
Kadiri siku zinavyozidi kwenda, ndivyo unapaswa kuwa bora zaidi, na kipimo ni ZAIDI LEO KULIKO JANA…

Jana ni karibu na rahisi kuiangalia, tuiangalie jana na tuhakikishe leo tunakuwa bora zaidi.
Angalizo; usije kujisahau na jana ikakupoteza, kwa sababu jana imepita, huwezi kuibadili. Ila leo unaweza kufanya makubwa, zaidi ya uliyofanya jana.

Nakutakia siku njema sana ya leo.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.