Hongera rafiki yangu kwa siku hii nzuri na ya kipekee sana kwetu.
Ni siku nyingine muhimu sana kwetu ambapo tunakwenda kuweka juhudi kubwa ili tuweze kupata matokeo makubwa sana.

img-20161217-wa0002
Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunajiweka kwenye nafasi ya kuwa bora zaidi kila siku.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu BEING USEFUL….
Chochote unachofanya kwenye maisha yako hakikisha kinakuwa cha maana, kinakuwa na msaada kwa wengine.
Kwa sababu chochote unachotaka sasa, utakipata kutoka owa wengine.
Unahitaji kuwa wa msaada,
Unahitaji kuongeza thamani kwenye maisha ya wengine.
Kwa njia hii wengine watakuwa tayari kukupa kile unachotaka.

Hii ndiyo kanuni ya uhakika kama mpaka sasa hujajua ufanye nini. Kama bado unajiuliza ufanye biashara gani, basi jibu la uhakika ni hilo, KUWA WA MSAADA, KUWA WA THAMANI KWA WENGINE.
Hakuna kitu kimoja ambacho kila mtu akifanya atafanikiwa, lakini kila mtu aja kitu chake ambacho akifanya anafanikiwa sana.

Chochote kitakachokuwa, hakikisha unakuwa wa msaada, unakiwa wa thamani, BE USEFUL.

Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.